Na, Mwandishi wetu, Geita
GEITA, Watu wawili wamefariki dunia kwenye ajali ambayo imehusisha gari la abiria aina ya (TATA) lenye namba za usajili T.422 DMQ mali ya kampuni ya SOMA lililokuwa likitokea Geita mjini kueleka Katoro pamoja na pikipiki iliyokuwa na abiria yenye namba za usajili MC 730 CLS aina ya Sanlg katika eneo la Mpomvu mjini Geita.
Waliofariki katika ajali hiyo hawaja fahamika majina yao ni dereva wa pikipiki pamoja na abiria wake mmoja ambao wote miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa utambuzi.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita kamishina Msaidizi wa Polisi Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo februari 24 majira ya saa 2:00 usiku huku akitaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva wa basi ambao ulipelekea kuigonga piki piki.
Kamanda Jongo alisema katika ajali hiyo, abiria wa pikiki hiyo amepata majeraha makubwa kichwani na kukatika miguu yote miwili na anaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Alisema dereva wa gari hilo alietambulika kwa majina ya Hakimu Changa (39) mkazi wa Mwanza, amekamatwa kwa mahojiano na hatua za uchunguzi zitapokamilika atafikishwa mahakani.

Comments
Post a Comment