WAZIRI BITEKO AKUTANA NA WATENDAJI WA TAASISI ZA WIZARA YA MADINI

MIKAKATI YA MABORESHO YA USIMAMIZI WA BIASHARA YA MADINI YAANISHWA 

Leo Juni 12, 2023 Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko jijini Dodoma, amekutana na  Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini kwa lengo la kuangalia namna bora ya kusimamia biashara ya madini hususan ya tanzanite na mengine ya vito sambamba na kuweka mikakati  ya kutangaza madini hayo  duniani.

Viongozi wengine wa Wizara waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, Wakuu wa Taasisi,  Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) na  Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI)

 _MIKAKATI YA MABORESHO YA USIMAMIZI WA BIASHARA YA MADINI YAANISHWA_ 

Comments