
Na Sumai Salum - Kishapu
Wanawake wajane wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wametakiwa kujipa moyo
na kupata muda wa kutosha wa kupumzisha akili kabla hawajaamua kuingia
kwenye mahusiano mengine mapya kwa lengo la kuondokana na changamoto na
migogoro ya mahusiano baada ya kuwa wameondokewa na wenza wao.
Hayo yamesemwa leo Juni 23,2020 na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri
ya Kishapu Bw. Joseph Swalala ikiwa ni siku ya maadhimisho ya Wajane
Duniani yenye kauli mbiu isemayo “HAKI NA ULINZI KWA WAJANE MSINGI IMARA
KWA MAENDELEO YA JAMII” ambapo ameiasa jamii kutoendeleza mila na
desturi kandamizi na zilizopitwa na wakati zenye lengo la kuwanyima
wanawake wajane haki zao za umiliki mirathi pindi wanapofiwa na waume
zao.
“Sheria ya mirathi inaeleza baada ya mme kufariki dunia mke anatakiwa
awe msimamizi ila mila na desturi kandamizi zimekuwa zikipindisha sheria
hii kwa kuchagua ndugu mme wa marehemu kuwa ndie msimamizi na mali
zikishaisha anamterekeza , lakini pia niwashauri wanawake wajane
wasiwahi kuolewa kwani wengi watakuja kwako kwa lengo la kufuja mali
kisha wanaondoka ni heri utulie kwanza ujue nini cha kufanya ili
kikusaidie wewe na watoto wako ulioachiwa”, aliongeza Swalala.
Pia Swalala alidai kuwa serikali inao utaratibu wa kutenga fedha aslimia
10 kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kuwaondolea liba tofauti na
awali ambapo wanawake ni (4%) ,vijana(4%) na watu wenye ulemavu (2%) kwa
lengo la kuwasidia kujiinua kiuchumi na kuongeza kipato huku akiziomba
taasisi na mashirika binafsi kwa kujitoa kwa wingi ili kuwawezesha
wajane.
Bi. Annastadhia Christopher Lwekila ambaye ni mjane anayeishi kijiji
cha Isoso kitongoji cha Karume ambaye ni mama mwenye watoto 5 aliyekaa
kwa miaka zaidi ya 6 bila mme wake na sasa anajishughulisha na ukulima
na utengezaji mapambo ya ndani, amesema kuwa wamekuwa wakikutana na
changamoto za kutaka kurithiwa baada ya kufiwa na waume zao huku wajane
wasio na watoto wakinyanyaswa na kufukuzwa kutokana na kuwa hawahesabiki
katika familia ya upande wa mwanamme huku akitoa wito kwa wanawake
kujishughulisha na biashara na kuondokana na utegemezi.
“Hali ya kunyanyaswa ipo kwa baadhi kwani siku ya matanga anachaguliwa
mtu wa kuilinda familia na baadae anatumia zile mali vibaya na matokeo
yake zikiisha basi anaondoka na kwa wajane ambao hawakubahatika kuzaa
yaani hawana thamani kabisa na mshukuru Mungu sasa nina uwezo wa
kujisimamia kiuchumi licha ya kuwa nina watoto wanaonitegemea sasa ni 2
kutokana na ukulima ninaoufanya pamoja na ususi za bidhaa mbalimbali za
asili najipatia kipato mbali na kuwa sikuwa nikijishughulisha mme wangu
kabla angali hai ila nawashauri jamii iwapende na kuwathamini wajane
lakini pia wanawake wafanye kazi hata kama bado wanawaume zao maana kifo
hakina hodi”, alisema Bi Lwekila.
Kivulini ni shirika linalotetea haki za wanawake na wasichana kwenye
mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Shinyanga katika wilaya ya Kishapu
ambapo Meneja miradi wa shirika hilo lisilokuwa la kiserikali Bi. Eunice
Mayengela amesema kuwa uwepo wa siku ya wajane inawapa fursa ya
kuendelea kuelimisha jamii juu ya haki sawa ya umiliki wa mali na kuwapa
kipaumbele kwa kuwasaidia wajane kwa kutatua changamoto mbalimbali
wanazopitia katika kipindi walipopoteza waume zao.
“Sisi kama shirika tuna haki ya kutetea wajane kwani imekuwa ni
changamoto kubwa hususa ni kwenye jamii ya kisukuma mara nyingi tumekuwa
tukiona baada ya kufariki mwanaume kunakuwa na migogoro huku mwanamke
akifariki hakuna migogoro na hiyo ni kutokana na mila na desturi
zinazoleta mitizamo mibaya na hata kunyanyaswa kingono wajane ili apate
huduma kutoka kwa msimamizi wa familia kwani hawana elimu ya kutosha juu
ya sheria ya mirathi ikiwamo muda wa kufungua shauri la mirathi
kufunguliwa baada ya siku 90 kuwa ni nyingi na hawana elimuya kumsaidia
piandi aonapo mali za marehemu zinatapanywa akaweke zuio mahakamani”
,alisema Bi. Mayengela.
Aidha Mayengela ameongeza kuwa ni wakati ambao jamii,watunga sera na
watoa maamuzi kuweka nguvu za pamoja kwa kusimamia maswala ya
upatikanaji haki za wajane kwa muda muafaka kwani mashauri mengi ya
mirathi yamekuwa yakichukua miaka mitano hadi kumi kukamilika jambo
ambalo kwa baaadhi ya jamii linalopelekea uvunjifu wa haki za wajane kwa
kitopewa nafasi za kusimamia mali walizovuna pamoja na waume zao kiasi
cha ndugu wa mwanaume kutapanya mali huku wajane na yatima wakihangaika
kimaisha.
Bwana Habibu Makusanya ni mkazi wa Kishapu ambaye amelaani mila na
desturi mbovu zinazo wanyima haki wanawake wajane ambao ndio
wanatakiwa kuwa walithi wa mali hizo ambazo walikuwa wakikusanya na
waume zao ili ziwasaidie wao na watoto waliochwa na baba wa familia huku
akiwashauri wanaume kuwa na mazoea ya kuandika wosia kwani itaondoa
utata wa kifamilia.
“Wito wangu ni kwa serikali ihakikishe inasimamia ulinzi wa wajane kwa
sheria za nchi ili wapewe haki za usimamizi wa mali za urithi bila
kuingiliwa na kubughuziwa na mtu yeyote,” Aliongeza Makusanya
Comments
Post a Comment