Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Magufuli ameacha neema katika shule ya sekondari Runzewe iliyopo Tarafa ya Siloka Wilaya ya Bukombe mkoani Geita kwa kutoa Tsh milioni 2 ikiwa milioni moja niya Rais Magufuli na milioni nyinginge alitoa Mama Janet Magufuli ili kuinua Elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Akikabidhi fedha hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba
baada ya muda mchache Rais Magufuli kutoa fedha hiyo wakati akihutubia wananchi
wa Kata ya Uyovu akielekea Wilaya ya Chato mkoani hapa.
Nkumba aliwataka walimu wa shule kutumia fedha hiyo kama
ilivyo elekezwa na kwamba wahakikishe wanatumia vyema fedha zote zinazotolewa
na serikali kwa maana ya kuinua taaluma ikiwemo kaptesheni ili wanafunzi wa
shule hiyo kuanzia kidato cha kwanza hadi
cha sita wanaendelea kufanya vizuri.
Aidha Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko
aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kuendelea na ushirikiano kwa kuwafundisha
wanafunzi ambao wanafanya vizuri kila mwaka hasa matokeo ya kidato cha sita.
Biteko aliwaomba walimu kufanya kazi yao ya kujitolea ili watengeneze kizazi
bora chenye maadili katika jamii itakayokuwa na tija katika ajira na sekta
binafisi.
Comments
Post a Comment