WIZARA YATOA KALENDA YA MIHULA YA MASOMO 2024

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania imetoa Kalenda ya mihula ya masomo kwa shule za awali, msingi na sekondari kwa mwaka 2024

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara, muhula wa masomo unatarajiwa kuanza Januari 8 na kukamilika Desemba 6, 2024.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa kutakuwa na jumla ya idadi ya siku za masomo 94 katika muhula wa kwanza utakaokamilika May 31 na siku 100 katika muhula wa pili utakaoanza Julai Mosi

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesisitiza utekelezaji wa Mihula ya Masomo kwa Mwaka 2024, kwa kuzingatia Kalenda hiyo ili kuepuka changamoto ya kutokamilisha ufundishaji na ujifunzaji wa mada kwa wakati.

Wizara imewatakia watu wote maandalizi mema na heri ya Mwaka mpya wa Masomo.


Comments