F. I. C YAHAMASISHA ELIMU KWA KUGAWA VIFAA VYA SHULE

 

Na, Ernest Magashi

Wananchama wa shirika la (F.I.C) yani Football International Charity  (F.I.C) Wamehamasisha Elimu kwenye jamii kwa kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Bulenga. 

Hayo yalisemwa na Wakala wa (F.I.C) Football International  Charity (F.I.C) kanda ya Bulega Ayoub Mwakalila wakati w akikabidhi msaada wa vifaa vya shule madafutari, na taulo za kike na vifaa vya michezo.
Pia alisema hawakuiacha mbali jamii yabwatu wenye ulemavu wa ngozi walipokea magodoro, huku wazee wenye umri wa miaka kuanzia 60 walipewa msaada wa braketi, sabuni, chumvi na mafuta ya kupaka.

Mwakalila alisema wameleta misaada mbalimbali na kuzikabidhi Vyenye thamani ya sh 2.7 milioni na kukabidhiwa kwa walengwa na diwani wa kata ya Bulenga Erick Kagoma ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.

Aliongeza kuwa wataendelea kufanya hivyo kwa maeneo mengine  ili kufikia malengo yao ya kufikia jamii na kuhakikisha inanufaika na misada ya wanachama wa F.I.C.
Mwanafunzi wa shule ya Bulega Sekondari Mhoja Joseph akizungumza kwaniba ya wasichana shulenihapo amesema wanashukru kwa Masada wa taulo za kike. 

Amesema hapo nyuma iliwalazimu kutohudhulia masomo wanapo ingia kwenye mzunguko wa mwezi lakini kupitia msaada huo unawafanya kuwa wajasili hata ikitokea wakiwa darasani wanauhakika watatoka na kurudi kuendelea na masomo.
Diwani ya kata ya Bulega Erick Kagoma wakati akikabidhi msaada wa magodoro na vifaa vya shule na taulo za wanafunzi wa kike vilivyo tolewa na shirika la (F.I.C) yani Football International Charity alisisitiza wazazi na walezi kupeleka watoto waliofikia kuaza shule waende kuadikishwa.
 
Kagoma akitoa shukrani kwa wadau hao ambao wameguswa na kutoa msaada kwa kuigusa jamii ameitaka kupeleka wa wanafunzi kidato cha kwanza na kwamba wazazi waone umuhiumu wa kuwekeza kwenye Elimu. 
Aliwapongeza pia wadau hao kwa kuwapa sabuni na chumvi wazee huku watoto wakiwakabizi magidoro ili kuboresha mazingira ya usingizi wao ikumbukwe vijijini kunawatito wanaishi maisha duni hivyo watu wa FIC mmefanya Jamboree kubwa kwa kushirikiana na serikali ambayo imekuwa ikifanya hivyo.
 

Comments

  1. Dhaaaaaaaaaaa walimu wetu wametisha xana ila pongezi nyingi ziende kwa mwl mwaka bravo kwako sir namukubali kinomaa

    ReplyDelete
  2. Nicheki WhatsApp wewe ambaye ni Mwalimu uweze kuwekeza katika Platform Bora ya FIC, kwa maelezo zaidi tuwasiliane call/WhatsApp 0736355806 wote mnakaribishwa

    ReplyDelete
  3. Lakini pia WhatsApp no: 0626689425 uweze kupata Link ya F.I.C uanze kuwekeza na kukuza Uchumi wako

    ReplyDelete

Post a Comment