Wanachama wa Football International Charity wameshelekea sikukuu ya krisimas na watoto yatima na wanaoishi mazingira magumu na kulelewa katika kituo cha Nyumba ya huruma.
Hayo yameelezwa na Wakala wa Football International Charity (F.I.C) Wilaya ya Bulombe Hussein Kulwa wakati akikabizi msaada wa magodoro, vifaa vya shule, na mchele, mafuta ya kula kwa ajili ya sikukuu ya krismas vyenye thamani ya sh 2.4 milioni katika kituo cha Nyumba ya huduma Ushirombo.
Kulwa amesema wameguswa kufanya hivyo ikiswa nisehemu ya kushirikiana na jamii katika mfanikio ya faida wanayo pata kupitia F.I.C na wezake.
Mlezi wa watoto kituo cha Nyumba ya huruma Rachel Ikenelwa na mwezake Sisita Elizabeth Bayo kwanyakati tofauti wametoa shukurani kwa wadau hao.
Rachel alisisitiza wadau wengine kuendelea kutembelea kituo hicho cha kulea watoto yatima na wanaoishi mazingira magumu na kusaidia mahitaji mbali mbali.
Sisita Elizaabeth amesema miongoni mwa watoto wanao walea niwanafunzi na wamekuwa wakifanya vizuri darasani hivyo wa naitaji misaada zaidi ili wafike malengo yao.
Miongoni mwa watoto wanao lelewa kwenye kituo hicho Neema Sungura aliwashukru waliowaletea mahitaji ya sikuu ya krisimas haliambayo itawafanya kushelekea kama watoto wengine.
Mkuu wa shule ya sekondari Businda Teodora Mushi akiwa na wadau wenzake wakitoa msaada huo aliwaomba watoto wanao soma na waliofikia umri wa kuadikishwa kuaza shule Januari wapelekwe ili waanze masomo.
MWISHO
Mbarikiwe katika kugusa hili nawao wamefarijika sana.
ReplyDeleteTuendelee kujitoa kwa moyo huo huo.
F.I.C HONGERA SANA ,PAMOJA NA WANACHAMA WOTE.
Amen, tuendelee kuwaunga mkono wenzetu
DeleteWell done by FIC community, together we can
ReplyDeletewell done
ReplyDeleteUpendo ni jambo la muhimu,hongereni sana
ReplyDelete