MAGUFULI : NILETEWE ORODHA YA VIONGOZI WANAOTUMIA LAINI ZA TTCL....HUWEZI KULIPWA MSHAHARA KAMA HUTUMII

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli amehoji juu ya Shirika la Mawasiliano la
Tanzania TTCL, kuwa na idaidi ya watumiaji wa simu wachache huku
watumiaji wa simu wakifikia milioni 40 nchi nzima.
Rais Magufuli amezungumza hayo kwenye
shughuli ya upokeaji wa gawio kutoka kwa shirika hilo, shughuli ambayo
imefanyika katika ofisi za makao yake makuu jijini Dar es salaam.
"Nakumbuka mwaka jana idadi ya wateja
walikuwa milion 1.8 lakini mmeongeza hadi kufikia milioni 2,
nawapongeza sana lakini narudia wito wangu kwa Watanzania kuwa rudini
nyumbani kumenoga", amesema Rais Magufuli.
"Pamoja na kwamba mmefanya mafanikio
makubwa, bado mna safari ndefu ili mufikie kuitwa Shirika la Mawasiliano
la Taifa, mnafahamu watu wenye simu nchini wanafikia milioni 40 nyinyi
mna watu Mil. 2.2 maanake soko lenu ni chini ya asilimia tano hamna budi
kuongeza bidii", ameongeza.
"Naomba niletewe orodha ya viongozi
ambao wanatumia laini za TTCL na sio ziwepo tu bila kutumika, huwezi
kulipwa mshahara wa serikali na hutumii mtandao huo, sijamaanisha
msitumie mitandao mingine"- amesema Rais Magufuli.
Comments
Post a Comment