
Na Issa Mtuwa. Dodoma
Waziri
wa madini Doto Biteko amewataka wafanyakazi wa wizara ya madini pamoja
na taasisi zake kufanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa wakati ili
kufikia malengo ya wizara hiyo.
Ameyasema
hayo jijini Dodoma wakati wa kikao chake na viongozi waandamizi wa
wizara ya madini na tume ya madini. Katika kikao hicho pamoja na mambo
mengine amezungumzia juu utekelezaji wa maagizo anayoyatoa na usimamizi
wa utekeleza wa maagizo yake. Ameongeza kuwa anawategemea sana viongozi
hao na wafanyakazi wote katika kufanikisha kazi na malengo ya wizara
hiyo.
Ametolea
mfano wa maagizo aliyowahi kuyatoa ni pamoja na ufutwaji wa leseni
zisizo hai ndani ya siku 7 na zingine siku 30 na lile linalo husu mgodi
wa North Mara kuhusu utiririshaji wa maji yenye sumu kwenda kwenye
makazi ya wananchi ambapo alitoa pia siku 30 kuhakikisha maji hayo
yanadhibitiwa.
Amewaambia
viongozi hao kuwa akishatoa maagizo, kazi ya kusimamia utekelezaji wa
maagizo hayo ni kazi yao. Amemshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa Tume
Prof. Idris Kikula na tume yake kwa kazi nzuri wanayoifanya na ziara
zake mikoani zimekuwa na tija.
Biteko
amesisitiza kuwa anatambua mchango wa watumishi wote wa wizara yake
hivyo amewaomba kuongeza bidii na kuongeza umakini katika utekelezaji
wa majukumu yao huku wakizingatia weledi na uadilifu.
Kikao
hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Katibu
Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila na Makamishna. Kwa upande wa
tume ya madini waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume Prof.
Kikula, Mtendaji mkuu wa tume ya madini Prof. Shukrani Manya, Mkurugenzi
wa Leseni Mhandisi Yahya Samamba, Mkurugenzi wa Biashara Dkt. Venance
Bahati.
Comments
Post a Comment