Waziri
wa Madini, Doto Biteko akishuhudia Mwakilishe wa Kampuni ya Barrick
Exploration African Limited (BEAL), Janet Lekashingo akipeana mkono na
mmiliki wa kampuni ya Megagems Tanzania Limited (MTL) baada ya kufikia
mwafaka wa mgogoro wao wa MTL kulipwa haki yake.
Waziri
wa Madini, Doto Biteko akipitia nyaraka iliyokabidhiwa kwake na
Mwakilishe wa Kampuni ya Barrick Exploration African Limited (BEAL),
Janet Lekashingo (hayupo pichani) kabla ya kumaliza mgogoro kati ya
Kampuni ya Barrick Exploration Africa Limited (BEAL) na Megagems
Tanzania Limited (MTL).
Waziri
wa Madini, Doto Biteko amemaliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Barrick
Exploration Africa Limited (BEAL) na Megagems Tanzania Limited (MTL) uliodumu
kwa muda mrefu.
MTL
ambaye ni mlalamikiji alikuwa anadai kulipwa kiasi cha Dola za Marekani 10,000 na
Kampuni ya BEAL.
Akisuluhisha
mgogoro huo Waziri Biteko ameitaka Kampuni ya BEAL kumlipa mlalamikaji kwa kuwa
vibali vyote vinaonesha kuwa anastahili kulipwa.
Kikao
hicho kimefanyika tarehe 25 Januari, 2019 jijini Dodoma katika Ofisi ya
Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Comments
Post a Comment