Wakati
vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi wa hali ya mtoto anayedaiwa
kufungiwa kabatini kwa miezi mitano, madaktari wametaja tatizo jingine
walilolibaini kwa mtoto huyo kuwa hatoi sauti.
Mtoto
huyo aliyelazwa wodi ya watoto wenye utapiamlo katika Hospitali ya Mkoa
wa Dodoma, amegundulika kuwa na tatizo la kutotoa sauti hata anapolia,
hivyo kuwafanya madaktari kuanza kutafuta sababu.
Akizungumza
na Mwananchi hospitalini hapo jana, Ofisa Muuguzi, Dina Msesa alisema
hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika baada ya kumwanzishia lishe ya
vyakula vya kuboresha afya yake, lakini tatizo lipo kwenye utoaji wa
sauti.
“Mtoto
huyu hatoi sauti yoyote wala halii, ila ametulia jambo linalofanya
wataalamu waanze kukuna vichwa kutafuta tatizo,” alisema Msesa.
Kuhusu
mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa mtumishi wa ndani, alisema afya yake
imeimarika na mkono uliokuwa umeumia umepona ambapo sasa anaweza
kuunyayua tofauti na awali.
Comments
Post a Comment