
Wapiga Debe wa Stand,timu ya Stand United al Maarufu kwa jina la Chama la Wana
imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka tanzania bara msimu wa
2018/19 kwa kuwapigisha kwata maafande wa JKT Tanzania kwa kuwachapa bao
1-0.
Mchezo
huo wa ligi kuu soka Tanzania bara umepigwa leo Januari 2 2019 katika
uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga mchezo ambao haukuwa na kasi
wala mvuto wowote kwa watazamaji katika kipindi cha kwanza kutokana na
wachezaji kukosa utulivu uwanjani (butua butua) kwa wachezaji kushindwa
kumiliki mpira hata kuchungulia nyavu zao.
Lakini
kipindi cha pili baada ya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji kutoka timu
zote mchezo ulishika kasi na wapiga debe wakafanikiwa kuwapigisha kwata
maafande wa JKT Tanzania kupitia mchezaji wake Moris Mahela mnamo
dakika ya 77 bao ambalo limedumu na kuwaibua vifua mbele wapiga debe
haona kufikisha jumla ya alama 22.
Kocha wa JKT Tanzania,Bakari Shime amesema
makosa yaliyojitokeza katika nafasi ya ushambuliaji ndio yamesababisha
kukosa alama tatu na kwamba watajipanga katika mzunguko wa lala salama.
"Kimsingi
wachezaji wameshindwa kutumia nafasi tulizopata,ambapo wenzetu wamepata
nafasi moja na kuitumia kupata alama tatu,sisi tunaendelea kujipanga na
michezo mingine ili kupata matokeo mazuri uwanjani", amesema Shime.
Upande
wapili kwa wapiga debe huku ni hoya hoya kwani chama la wana limekuwa
likisuasua kupata matokeo mazuri katika dimba la kambarage kocha
Athuman Bilal amesema kazi imeanza na timu ipo tayari kuleta ushindani
katika mzunguko wa pili.
Comments
Post a Comment