Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi
kuzingatia kanuni,sheria na miongozo ya Uchaguzi wanaposimamia na
kutekeleza majukumu ya uchaguzi.
Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh. Jaji Mstaafu
Mery Longway katika ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi na wasimamizi
wasaidizi wa Uchaguzi yaliyofanyika Mkoani Dodoma leo.
Ameeleza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndio yenye jukumu la kusimamia ,
kuendesha na kuratibu Uchaguzi , lakini wanaosimamia jukumu hilo kwa
ukaribu zaidi ni wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo , Wasimamizi
wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata
pamoja na Watendaji wa vituo vya kupigia Kura.
“Nawakumbusha kuzingatia kanuni, Sheria na Miongozo yote iliyotolewa
na itakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kusimamia jukumu hili
kwa ufanisi na mafanikio makubwa”. Amesema Mh. Longway.
Aidha amewakumbusha wasimamizi hazo wa Uchaguzi kuwa Uchaguzi ni
Mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kufuatwa na
kuzingatiwa ndio msingi wa Uchaguzi kuwa huru wa haki na kupunguza kama
siyo kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa Uchaguzi na
hivyo kupunguza kesi mahakamani baada ya Uchaguzi.
Amesema kuwa pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo kuwa wazoefu
katika kuendesha Uchaguzi washiriki hao wametakiwa kuhakikisha
wanazingatia maelekezo watakayopewa na wakufunzi wa Tume, haitokuwa
vyema kutekeleza majukumu hayo kwa mazoea bali wanatakiwa kuzingatia
matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni zinazosimamia zoezi la Uchaguzi
Washiriki wa Mafunzo hayo ni Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo ,
Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi
ngazi ya Kata ambao watasimamia Uchaguzi Mdogo wa Umbunge Jimbo la
Temeke na Udiwani katika kata 46 utafanyika Januari 19 mwaka 2019.
Comments
Post a Comment