Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Amri Jeshi Mkuu, Dkt. John Magufuli ametoa salamu za Kumbukumbu ya
Miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara, leo Ijumaa, Desemba 7, 2018 Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Akituma salam hizo, Rais Magufuli kwa
mujibu wa Ibara ya 45 Ibara ndogo ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, ametangaza msamaha kwa wafungwa 4,477 waliokuwa wamefungwa /
kuhukumiwa kwenye magereza mbalimbali nchini ambapo kati yao 1,176
wataachiwa Desemba 9, 2018 katika Sikukuu ya Uhuru.
“Wafungwa 1,076 watatoka siku ya
Maadhimisho ya Uhuru yani December 9, 2018, msamaha huu utawahusu
Wafungwa Wagonjwa, Wazee kuanzia miaka sabini na zaidi, Wafungwa wakike
walioingia Gerezani wakiwa Wajawazito”
“Nimeamua Wafungwa waliotumikia robo ya
adhabu zao wapunguziwe robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la
theluthi moja” -Rais Magufuli
Comments
Post a Comment