
Mkuu wa Jeshi la Polisi chini, IGP Simon Sirro.
Mkuu wa Jeshi la Polisi chini, IGP Simon
Sirro amefanya mabadiliko katika jeshi hilo na kuwabadili baadhi ya
makamanda vyao vya kazi akiwemo RPC wa Mtwara Lucas Mkondya.
Akizungumza na wanahabari leo, jijini
Dar es salaam, aliyekuwa Kamanda wa Polisi jijini Mwanza, Ahmed Msangi
ambaye sasa amekuwa Mkuu wa kitengo cha Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi akichukua nafasi ya Msemaji wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa,
amesema mabadiliko hayo ni ya kawaida.
Kamanda Msangi amesema kuwa, "Aliyekuwa
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Barnabas Mwakalukwa, anakwenda kuwa
Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Pwani huku aliyekuwa mnadhimu wa Pwani sasa
anakwenda kuwa RPC wa mkoa wa Mtwara akichukua nafasi ya Lucas Mkondya
aliyehamishiwa kitengo cha Intelijensia ya Makosa ya Jinai Makao Makuu
Dar es salaam".
Comments
Post a Comment