
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
inapenda kuwajulisha Wananchi wote kuwa; imefungua Dawati maalumu la
Usajili wa Vitambulisho vya Taifa na kushughulikia maombi yote ya haraka
kwa wateja wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wenye
hitaji la kufungua Kampuni, Kusajili Nembo za Biashara n.k
Huduma hii ya haraka (Fast Tracking)
inatolewa kwenye ofisi zote za NIDA zilipo nchi nzima. Muhimu kuwa na
nyaraka za Utambulisho zinazoonyesha hitaji la kufungua Kampuni au
kusajili Nembo ya Biashara kulingana na utaratibu utakao elekezwa kwenye
kituo chetu.
Kwa wateja ambao hawajaanza taratibu za
Usajili wa Vitambulisho vya Taifa mnashauriwa kuanzia Serikali ya
Mtaa/Kijiji unakoishi, kujaza fomu ya maombi ya Vitambulisho vya Taifa
na kufika kwenye ofisi zetu kwa hatua ya kupiga picha, na kuchuliwa
alama za vidole. Muhimu kuzingatia taratibu zote za Usajili na Utambuzi
ni lazima zifuatwe kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya
Usajili.
Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0673 – 333444.
Limetolewa na;
Akital
Dkt. Arnold Kihaule,
MKURUGENZI MKUU
19 NOVEMBA 2018
Vitambulisho vyetu lini vitakua tayari
ReplyDelete