PWANI YAJIPANGA KUKUZA ZAO LA MUHOGO

Afisa Kilimo Wilayaya Kibiti Bwenda Ismail (kulia) akiwa na AfisaUgani wa wilaya hiyo Organess Semwenda wakiangalia muhogo unaolimwa katika shamba la Kibiti Farm Estate lilipo kata ya Bungu wilaya ya Kibiti.
Meneja wakiwanda cha kusindika muhogo cha Ukaya kilichopo Mkuranga Joseph Mtanga (kulia) akimueleza Afisa Mazao wa Wilaya hiyo  Derick Samuel namna kiwanda chake kilivyokwama kuendelea nauzalishaji kutokana na kukosekana kwa umeme.
Baadhi ya wakulima wa zao la muhogo wilaya ya Mkuranga wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Munir Shemweta, Pwani

Mkoa wa Pwani umeanza uhamasishaji wa uwekezaji katika zao la muhogo ili kuwawezesha wakulima kujiongezea kipato sambamba na kuendanana soko la China ambapo Tanzania imepata fursa kuuza muhogo nchini humo.

Hali hiyo imebainika mwishoni mwa wiki wakati maofisa kutoka Wizara ya Kilimo walipotembelea mkoa huo ikiwa ni mkakati wa wizara kuhamasisha ulimaji zao la muhogo na kuangalia changamoto zake kwal engo la kuongeza tija na uzalishaji waza ohilo.

Akielezea  harakati  za wilaya ya Kibiti  katika  kuhamasisha zao la muhogo Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Bw. Bwenda Ismail alisema, uhamasishaji huo unaenda sambamba na utoaji mafunzo, utoaji mbegu bora kwa wakulima pamoja na kuhakikisha kila kaya inakuwa na hekari moja ya muhogo jambo litakaloongeza uzalishaji. Kwa mujibu wa Ismail sasa hivi zao la muhogo katika wilaya ya kibiti limekuwa la kibiashara na hali hiyo inatokana na usafirishwaji wa muhogo mbichi kwa wingi kila siku kutoka wilaya hiyo kuenda dar es salaam.

Alisema kuwa, hatua nyingine inayofanywa na halmashauri ya wilaya ya Kibiti ni kusaidia  wakulima katika uuzaji muhogo hasa baada ya kubainika wakulima katika wilaya hiyo wamekuwa wakipunjwa wakati wakuuza muhogo kwa wafanyabiashara na sasa wilaya imejenga soko la pamoja lililogharimu milioni 65 na mategemeo ya wilaya ni kuwa muhogo utauzwa kwa vipimo stahiki tofauti na sasa ambapo wakulima wanapunjwa kwa mihogo kutenganishwa ile mikubwa na midogo.

Afisa kilimo huyo wa wilaya ya Kibiti alisema, uhamasishaji umewekwa pia katika ujenzi wa viwanda lengo likiwa kuhakikisha muhogo unaonunuliwa kutoka kwa wakulima unasindikwa sambambana kuhakikisha wilaya kibiti m inatenga maeneo kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi, wawekezaji wakubwa, wakati na wadogo pamoja na maeneo kwa ajili ya vijana na msisitizo ukiwa kila kata itenge eneo.

Kwa sasa Wilaya ya Kibiti umekamilisha sheria ndogo ambapo kila kaya itatakiwa kulima zao la muhogo jambo litakalosaidia kusukuma watu kuingia shambani ikiwemo vijana ambapo sasa watalazimika kuingia katika kilimo ili kuendana na kasi ya Tanzania ya viwanda na soko la china la muhogo kwa kuzalisha muhogo wa kutosha.

Kwa upande wa wilaya ya Mkuranga, serikali wilayani humo katika bajeti yake imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kununua na kusambaza mbegu za muhogo kwa wakulima mbalimbali. Afisa Kilimo wilayani humo Bi. Julita Bulali amebainisha kuwa kutokana na jitihada za kusambaza mbegu kwa wakulima kumekuwa na mwitikio mkubwa wa watu kuwekeza katika zao la muhogo.

Hata hivyo, changamoto kubwa katika wilaya hiyo ni kusitishwa kwa huduma katika kiwanda cha Ukaya farm ambacho imekuwa mkombozi mkubwa wa kununua muhogo kutoka kwa wakulima kutokana na kukosekana kwa umeme katika kiwanda hicho.

Kwa mujibu wa meneja wa kiwanda hicho bw. Joseph Mtanga, awali kiwanda hicho kilikuwa kikitumia jenereta lakini mara baada ya kuharibika najitihada za kupataumeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kushindikana shughuli za kiwanda zimesimama na hivyo kuwakosesha wakulima kuuza muhogo katika kiwanda hicho. 

Meneja huyo wa kiwanda cha Ukaya Farm alisema kiwanda chake hununua wastani wa tani nne mpaka mpaka kumi na mbili kwa siku kutoka kwa wakulima na kusitishwa kwa usindikaji kumesababisha pia ajira za watu thelathini mpaka arobaini kusimama.

Baadhi ya wakulima mkoani humo walisema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa soko la uhakika jambo linalosababishwa mzunguko wa biashara kutoenda vizuri.

Walisema biashara ya muhogo wakati mwingine inakwama kutokana na masuala ya kisera ambapo bidhaa zao zinahitaji kuhalalishwana shirika la viwanga Tanzania (TBS) jambo linalofanya kushindwa kuingia katika ushindani kutokana na kutokidhi vigezo. Pia ukosekanaji wa vipimo stahiki katika uuzaji muhogo katika magari unawanyonya wakulima kwa kuwa bei wanayakubaliana mazao yakiwa shambani tofauti nabei wanayouza.

Comments