SERIKALI
ya Ufaransa imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa mapambano dhidi ya
rushwa na inaamini fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali zitatumika kama ilivyokusudiwa.
Kauli hiyo imetolewa leo
(Jumatatu, Machi 05, 2018) na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Bw.
Frederic Clavier alipomtembelea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye
makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Balozi Clavier amesema Ufaransa imeridhishwa na mapambano ya rushwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wataendelea kushirikiana nayo katika uboreshaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pia Balozi huyo amesema Septemba mwaka huu wanatarajia kufungua ofisi ya Shirika la Kimataifa la Misada ya Maendeleo la Ufaransa (AFD) jijini Dar es Salaam ili kurahisisha utoaji wa huduma. Kwa sasa ofisi za AFD zipo Nairobi nchini Kenya.Shirika hilo limekuwa likishirikiana na Serikali, katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo na ya maji safi na maji taka kwenye mikoa ya Simiyu, Mwanza, Musoma na Morogoro.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka
kipaumbele katika uwajibikaji na kupambana na rushwa ili kuhakikisha
fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi zinatumika vizuri
pamoja na wananchi kupata haki.
Amesema
mapambano dhidi ya rushwa yataiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya
kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda, uwekezaji, kilimo na utalii,
hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha
wawekezaji kutoka nchini Ufaransa ili waje kuwekeza kwenye ujenzi wa
viwanda, kilimo, madini na miundombinu mbalimbali.
Pia
Waziri Mkuu amesema Serikali itashirikiana na Ufaransa katika kuandaa
mikutano mbalimbali itakayowakutanisha wadau wa sekta binafsi kutoka
nchi zote mbili ili kuwapa mbinu za namna ya kukuza uchumi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini
Tanzania, Frederic Clavier, kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay
jijini Dar es Salaam, Machi 5, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini
Tanzania, Frederic Clavier, kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay
jijini Dar es Salaam, Machi 5, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa
Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier (katikati), kwenye makazi ya
Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Machi 5, 2018, kushoto ni
mwakilishi mkazi wa Nchi ya Ufaransa, Emanuel Baudran. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Comments
Post a Comment