Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na wadau wa sekta ya pamba kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkoa huo. |
Wakuu wa Wilaya za Mbongwe,Chato na Bukombe wakimsiliza Mkuu wa Mkoa wakati wa kikao cha wadau wa Sekta ya pamba mkoani Geita. |
Katibu tawala msaidizi idara ya uchumi na uzalishaji mkoani humo Emily Kasagara,akielezea mikakati ya utekelezaji wa kilimo cha pamba Mkoani Geita. |
Wenyeviti wa Halmashauri za Geita Mji,Geita DC,Mbongwe na Bukombe wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu tawala msaidizi idara ya uchumi na uzalishaji mkoani humo Emily Kasagara. |
Wakati serikali Mkoani Geita ikiendelea kujidhatiti vyema
kurudisha hadhi ya kilimo cha pamba Imebainika
kuna watu wachache ambao wameendelea kuzorotesha jitihada za kilimo cha
zao hilo la biashara kutokana na baadhi ya wataalamu kuchukua dawa za viuwatirifu
na kuzipeleka kwenye maduka ya kilimo
kwa ajili ya kuuzwa kwa Bei kubwa.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi wakati wa
kikao cha wadau wa kilimo cha pamba mkoani humo ambacho kilikuwa kimelenga kutathimini usambazaji wa viuwadudu pamoja na
maandalizi ya soko la msimu wa pamba
ambalo linaanza mwezi mei.
Ambapo alisema
serikali haiwezi kuwavumilia watu ambao wamekuwa wakirudisha nyuma jitihada za
ulimaji wa zao hilo.
“Kuna watu
wachache ambao hawana nia njema na mpango huu dawa zinaweza zikapotea njiani
zikaingia bahati mbaya kwenye maduka ya jumla na mtumishi yoyote tutakaye
mkamata hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa mara moja serikali imewekeza
fedha nyingi na hivi viuadudu ni vidogo
tu lakini kwa sababu ya tamaa baadhi ya watu wamekuwa wakivipeleka kwenye
maduka ili viuzwe bei ghali tutaanza kufanya uhakiki wa haraka”Alisisitiza
Luhumbi.
Luhumbi
ameongeza kwa kuwataka wakulima kuondokana na dhana ya kuweka fedha ndani na badala
yake watumie asasi za kifedha yakiwemo mabenki kuweka fedha zao kwani kufanya hivyo itawasaidia
kuweka sehemu salama na kuepukana na vitendo vya kuendelea kuibiwa pindi
wanapokuwa wameuza mazao yao.
Aidha Samweli
Shangembe ambaye ni Mkulima wa pamba Wilayani Chato ,alisema utaratibu ambao umewekwa wa kufungua
akaunti ni mzuri ila ameiomba serikali kutoa waraka kwenye uongozi wa vijiji ili
waweze kuwahamasisha wakulima wote ambao wamelima zao la pamba waweze kufungua
akaunti.
Kwa upande
wake Katibu tawala msaidizi idara ya uchumi na uzalishaji mkoani humo Emily
Kasagara alisema Katika msimu wa kilimo 2017/18 Mkoa ulilenga kulima hekta elfu
sabini na nane miatano arobaini na tisa
(78,549) ambazo ni sawa na ekari laki moja tisini na sita elfu miatatu sabini
na tatu ( 196,373) ambazo zinatarajia
kutoa mavuno ya tani elfu tisini na nane mia moja tisini na sita nukta tano (98,196.5.)
Comments
Post a Comment