Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Rulegea na viongozi wa chama cha mapinduzi(CCM)wilaya ya Geita wakishiriki kuchimba msingi kwaajili ya Ujenzi wa shule ya Msingi Kijijini Hapo. |
Afisa Elimu wa kata ya Izumacheli Bw Thomson Jerusinga,akisoma taarifa ya Ujenzi wa shule hiyo. |
Diwani wa Kata ya Izumacheli, Bw Ismail Manyama akisisitiza wananchi kushirikiana kwenye shughuli ya Ujenzi wa shule. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisiza wananchi kuwa wamoja na kushirikiana na serikali ili waweze kumaliza ujenzi wa Shule. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herma Kapufi pamoja na wananchi wakishiriki kuchimba Msingi kwaajili ya ujenzi wa shule. |
Kufuatia
ajali ya maji iliyosababisha vifo vya wanafunzi watatu (3) wakati wakitoka
shuleni mnamo Mei 22 mwaka jana(2017) kitongoji cha Rulegea, kijiji cha Butwa
Kata ya Izumacheli wilayani Geita, wananchi wa eneo hilo wameanzisha ujenzi wa
shule kwa lengo la kuwaepusha wanafunzi na kusafiri majini umbali mrefu kufuata
Elimu.
Katika
ujenzi huo wananchi hao wanashirikiana na mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl. Herman
Kapufi na viongozi wa chama cha mapinduzi(CCM).
Hatua hiyo
inatokana na wanafunzi kuendelea kupata shida ya kuvuka mara kwa mara pindi
wanapokwenda na kutoka shuleni kwa kutumia mitumbwi hivyo kuhatarisha maisha
yao.
Afisa Elimu
wa kata ya Izumacheli Bw Thomson Jerusinga alisema tatizo la watoto kuvuka maji
mara kwa mara limesababisha wananchi wengi kuhama kijijini hapo.
“Kabla ya
tukio la Mei 22 mwaka jana kitongoji hiki kilikuwa na Kaya 184 lakini baada ya
lile tukio la kuzama wanafunzi, wananchi wengi walihama kwa hiyo ikasababisha kuwepo
kwa Kaya 60 badala ya mia moja themanini na nne(184). Eneo ambalo tunatarajia
kuanza ujenzi litaweza kujenga vyumba vya madarasa pamoja na ofisi za walimu na
viwanja vya michezo”Alisema Jerusinga.
Diwani wa
Kata hiyo Bw Ismail Manyama alisema wanafunzi wa eneo hilo wameendelea kupata
shida kutokana na kuvuka maji hivyo kukamilika kwa shue hiyo kutawasaidia
kuepuka kwenda kijiji jirani.
Aidha Mkuu
wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi aliwasisitiza wananchi hao kuwa wamoja ili
waweze kufanikisha ujenzi huo wa shule pamoja na Nyumba za walimu na kwamba
serikali ipo nao bega kwa bega kuhakikisha kwamba wanafanikisha Ujenzi huo.
Nae
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita, Bw Barnabas Mapande
amewataka wananchi hao kutowasikiliza watu wanaowapotosha katika kushiriki
shughuli za maendeleo kwani kufanya hivyo ni kuweka hazina kwa vizazi vilivyopo
na vijavyo.
Baadhi ya
wananchi wa eneo hilo wamesema kuna kila sababu ya kushirikiana na viongozi wao
kujenga shule hiyo kwa manufaa ya watoto wao
Comments
Post a Comment