Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa wito huo Machi 12, 2018 kwenye
mkutano na wananchi hao uliofanyikia kwenye Kitongoji cha Mahiga na
kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali wa Serikali.
Mkutano
huo unafuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Magufuli alilolitoa Machi 11, 2018 kwenye mkutano na wananchi wa
Kahama ambapo alielezwa na Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum kuwa
wananchi wa Mahiga wana mgogoro wa muda mrefu na mwekezaji hususan
kuhusiana na suala la ulipaji fidia ili kupisha mradi.
Kufuatia
maelezo hayo ya Mbunge, Rais Dkt. Magufuli alimuagiza Naibu Waziri
Biteko kuhakikisha anafika kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi na
kuwasikiliza wananchi.
Rais
Magufuli alisisitiza kuwa ni wakati sasa Watanzania waanze kunufaika na
rasilimali zao ikiwemo madini. "Tunataka madini yawanufaishe
Watanzania," alisema Rais Magufuli.
Alisema
wawekezaji wakifika nchini ni lazima wahakikishe Watanzania wananufaika
kwa namna mbalimbali ikiwemo ajira, kodi na tozo.
"Jukumu
langu nimeamua kusimamia suala hili; Nawahakikishia Serikali iko imara
kwa ajili ya kuwatetea wanyonge," alisema Rais Dkt. Magufuli.
Aliagiza
mwekezaji atakayehitaji kuchimba kwenye maeneo yenye wachimbaji wadogo
ni lazima kwanza akubaliane nao ikiwemo suala la ulipaji wa fidia na sio
kuwafukuza.
"Suala la
wachimbaji lizingatiwe kwa mujibu wa sheria. Tuwalee ndio maana
tumeanzisha vituo vya mfano maeneo mbalimbali ili wajifunze," alisema.
Aidha,
kwa mujibu wa Mbunge huyo ni kwamba mgogoro huo ulianza tangu Julai 2017
baada ya mwekezaji huyo kuanza shughuli zake za kuandaa mazingira ya
kuchimba bila kuwa na makubaliano maalum na wananchi hao.
Akiwa
katika mkutano na wananchi hao, Biteko alielezwa kero mbalimbali
zinazowakabili ikiwemo kutoridhishwa na kiasi cha fidia kilicholipwa ili
kupisha maeneo yao kwa ajili ya mwekezaji, wengine kutohitaji kabisa
fidia na maombi ya baadhi yao kuruhusiwa kufanya shughuli mbalimbali
ikiwemo kilimo, ufugaji na uchimbaji kwenye maeneo husika.
Biteko
aliwataka kufanya subira wakati Serikali inatazama namna bora ya utatuzi
wa hoja zao kwa mujibu wa sheria ili manufaa yapatikane bila kumuonea
yoyote.
Alisema Rais Dkt. John Magufuli anataka kuona Watanzania wanyonge wananufaika na rasilimali zao ikiwemo rasilimali madini.
“Serikali
ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ni Serikali
inayowaangalia wanyonge. Nimesikiliza kero zenu nitazifikisha na hatua
itachukuliwa kwa mujibu wa sheria. Mfanye subira," alisema Biteko
Aliongeza kuwa Serikali haipo tayari kuona Watanzania wanyonge wanateseka na kwamba wakati umefika wa wao kunufaika.
Alifafanua kuwa suala lao litashughulikiwa kwa wakati na kwa kuzingatia Sheria ili haki itendeke pasipo kumuumiza yoyote.
Hata
hivyo aliwakumbusha wananchi hao kuhakikisha wanafuata utaratibu na
sheria ili manufaa yapatikane bila kuleta madhara yoyote.
Aidha,
kwa mujibu wa Mthamini wa Wilaya ya Shinyanga, Devotha Njella ni kwamba
wananchi waliofanyiwa tathmini ni 500 na kwamba bado mwananchi mmoja
mwenye heka 25 na nyumba 6 ambaye alikataa.
Alifafanua
kwamba malipo hayo ya fidia yalifanyika kwa awamu mbili na kwamba
katika awamu ya kwanza Shilingi 953,194,050.75 zililipwa na awamu ya
pili kiasi kilicholipwa ni Shilingi 472,413,686.32 na kwamba bado kiasi
cha Shilingi 208,886,951.01 ambacho taratibu za kulipa zinaendelea.
Comments
Post a Comment