Diwani
wa Kata ya Haneti Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Peter Elia
Chidawali akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari
Haneti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni
ijulikanayo ‘Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima’
Wilayani Chamwino.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja akitambulisha Kampeni ya
Kitaifa ya Kuzuia Mimba za Utotoni kwa wanafunzi wa shule sambamba na
utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatil idhidi ya
Wanawake na watoto katika Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Shukuru
Shanjala akiwaasa watoto wa kike kujitambua na kujilinda dhidi ya mimba
za utotoni ili kupata haki ya kuendelezwa na kutoa mchango katika
kufikia uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya kuzuia mimba za utotoni Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma
wakisikiliza ushauri wa malezi na makuzi kutoka kwa wataalamu jinsia ili
kuwawezesha kupambana na mimba za utotoni wakati wa uzinduzi wa kampeni
ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua
Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Afisa
Maendeleo Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule
ya msingi na sekondari Haneti Wilayani Chamwino kuhusu kupambana na
Mimba za utotoni katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni
ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani
humo.
Afisa
Maendeleo Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akitoa vipeperushi kwa wanafunzi wa
Shule ya msingi na sekondari Haneti Wilayani Chamwino kuhusu kupambana
na Mimba za utotoni katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za
Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima
Wilayani humo.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma
wakisoma vipeperushi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za
Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima
Wilayani humo.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma
wakionesha vipeperushi mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba
za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango
Mzima Wilayani humo.
Diwani
wa Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali(wanne kulia) akiwa katika
picha na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Rose Minja(wa
tatu kulia) pamoja na waalimu na wanafunzi wa shule ya msingi na
sekondari Haneti mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za
Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima
Wilayani Chamwino.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma imejipanga kupambana na kutokomeza mimba za utotoni katika Wilaya hiyo.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Kapeni ya Kutokomeza Mimba za Utotoni katika Shule
za Msingi na Sekondari katika Kata ya Haneti Wilayani Chamwino Diwani wa
Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali amesema kuwa Kata yake na
Wilaya kwa ujumla wamejipanga katika kupambana na vitendo vya ukatilia
wa kijinsia yakiwemo matukio ya mimba na ndoa za utotoni .
Mhe.
Peter Elia Chidawali ameongeza kuwa hawatakubali kuona watoto wao
wanapoteza haki yao ya msingi ya kuendelezwa ya kupata Elimu kwa kupata
mimba au kuolewa wakiwa bado shuleni.
“Tutaendeleza
Kampeni katika ngazi za familia kwa kuwaelimisha wazazi na walezi
kuhusu madhara ya mimba za utotoni ili tuokoe kizazi cha kesho”alisema
Mhe. Chidawali.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja amesema kuwa
suala la mimba za utotoni limezidi kuongeza siku hadi siku hivyo basi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alizindua
Kampeni ya Kutokomeza Mimba za utotoni kwa lengo la kuwezesha utoaji wa
elimu kwa wanafunzi, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushiriki
mapambano dhidi tatizo hili.
“Wanafunzi,
Walimu, Wazazi na walezi tuweke mikakati thabiti ya kupambana na tatizo
hili la mimba za utotoni” alisisitiza Bi. Rose.
Kwa
upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Chamwino Bi. Shukuru Shanjala ameeleza kuwa Wilaya ya Chamwino
imejipanga katika kuzuia mimba za utotoni kwa kuhakikisha wanawafikia
wahusika katika ngazi za shule na familia na kutoa elimu kwa watoto wote
wa kike wanaowazunguka ili kuondokanana tatizo la mimba za utotoni
katika wilaya yao.
Comments
Post a Comment