Katibu msaidizi wa Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo,Bw Gregory Kibusi akijitambulisha na kuelezea lengo ambalo limewapeleka Mkoani Geita mbele ya Afisa madini wa Mk0a huo. |
Afisa madini Mkoa wa Geita,Mhandisi Ally Maganga akizungumza na Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo ambao walikuwa wamewasili kwenye ofisi za madini Mkoani Humo. |
Bw,Nuru Shabani ambaye ni mchimbaji mdogo akionesha kemikali ambayo amekuwa akiitumia kukamatia madini kwenye eneo la mgodi wake. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita ambaye pia ni mchimbaji ,Bw Leornad Kiganga Bugomola akiwakaribisha wajumbe kwenye mkutano wa wadau wa madini. |
Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale ambaye pia ni mchimbaji na Mjumbe kwenye kamati hiyo,Hussen Nassoro Kasu akiwataka wachimbaji kuendelea kuwa wamoja na kushirikiana kwenye shughuli zao. |
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakiwa kwenye kikao hicho.
Na,Joel Maduka,Geita
|
Serikali kupitia Shirika la Viwango nchini, TBS limetakiwa
kuchunguza kemikali bandia zinazouzwa na
wafanyabiashara wasio waaminifu kwa wachimbaji wadogo wa madini hali
inayosababisha hasara kwa wachimbaji hao.
Rais wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini, (FEMATA)
Bw John Bina amesema hayo baada ya kikao kilichowakutanisha wachimbaji wadogo
Mkoani Geita kwa lengo la kujadili namna Serikali inavyoweza kufanikisha ujenzi
wa soko la madini kwa kanda ya ziwa.
Alisema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza
kemikali bandia kwa wachimbaji wadogo na
hivyo kuwasababishia hasara.
“Tunaomba serikali na TBS kuangalia sanaa haya madawa ambayo
yanaingia nchini kuhakikisha wanachunguza kemikali hizi kwani kwa sasa
uzalishaji unashuka kwa kiasi kikubwa wa madini ,na nyie wachimbaji niwaombe
muwe mnachunguza kabla ya kununua kwani kweli mnaingia hasara kubwa sanaa”Alisisitiza
Bina.
Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Bw Nuru Shabani alisema kwa kuuziwa Kemikali hizo bandia
amekuwa akiathirika katika shughuli zake.
“Kiukweli tunaathirika sanaa na hili halina ubisha sasa hivi
unaweza kununua tani moja ya kaboni unakuta inapitisha bila ya kushika mali
inamaana hadi iwe na pipim kuanzia mia saba hadi mia nane ,Ila kwa sasa
nashukuru walau serikali imetambua mchango wetu na imetuthamini mimi nilikuwa
naomba kupitia Kitengo chetu tuwe na wasimamizi ambao watatusaidia kubaini
kemikali hizi”Alisema Nuru.
Bw John Bina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
kushughulikia kero za wachimbaji wadogo alisema pamoja na matatizo hayo lakini wachimbaji hao wamekubaliana kuanzishwa kwa
soko la madini Mkoani Mwanza ili kudhibiti vitendo vya utoroshwaji wa madini.
Comments
Post a Comment