Mbunge
wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ametoa ratiba ya majeruhi wa
shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha ambao walikuwa nchini Marekani
kimatibabu kufuatia ajali walioipata.
Mhe. Nyarandu kupitioa ukurasa wake wa instagram ameweka ratiba hiyo
kuwa watapitia katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) ambapo mgeni
rasmi atawasili saa mbili asubuhi.
RATIBA ya MAPOKEZI KIA: Familia na Wananchi wanatarajiwa KUWASILI KIA
saa 3 asubuhi, Mgeni Rasmi atawasili saa 2 asubuhi, na Ndege aina ya
DC-8 inayowaleta WATOTO itakua saa 3 asubuhi. Hafla itafanyika KIA,
upande wa Magharibi mwa UWANJA kupitia VIP. Wote mnakaribishwa! Kesho
nitatoa RATIBA ya vile HAFLA ya uwanjani itakavyofanyika. (Mapema leo
nilitembelea KIA kushiriki kupanga ITIFAKI na MPANGILIO wa HAFLA
utakavyokuwa, na tayari nimempokea Daktari Bingwa Steve Meyer (akiwa
n.a. mke wake Dana Meyer) aliyeongoza matibabu ya WATOTO, sote tukiwa
tayari kwa mapokezi.KARIBUNI sana!
Watoto hao Doreen Wilson na Sadia wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa hii Augost 18, 2017 ambapo watapokelewa katika uwanja huo.
Comments
Post a Comment