
Baadi ya wananchi wakiondoa paa la bai ili kuokoa watu waliokuwa kwenye nyumba iliyoangukiwa na mti usiku wa kuamkia leo
Na,Vero Ignatus,Arusha
Kutokana
na mvua inayonyesha mfululizo Mkoani Arusha imeleta maafa makubwa
katika familia ya mzee Jonathani Kalambiya(55) mkazi wa sokoni II katika
kijiji cha kinyeresi wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya mti mkubwa
uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote
watano.Mkasa huo wa kusikitisha ulitokea jana majira ya saa 7 usiku
baada ya mti huo kung’olewa na maji uliangukia nyumba hiyo iliyokuwa
jira na mti huo.Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja watoto waliokufa katika
tukio hilo ni pamoja na watoto wawili wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni
mlinzi wa hospital ya ya Dr Mohamed ya Jijini ArushaMkumbo aliwataka
wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya tukio alikuwa
kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa kidatu cha pili
wa shule ya sekondari ya Inaboishu.Kamanda alimtaja mwanafunzi mwingine
ni ambaye ni mtoto wa mzee huyo ni Grolia Jonathani(11) mwanafunzi wa
shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha.Amesema
watoto wengine wa mzee huyo ni pamoja na mtoto wa kwanza wa mzee huyo
aliyetambuliwa kwa jina la Giliad Jonathani(31),Lazaro Lomnyaki (26) na
Best Jonathani(20).
Kamanda
Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana
uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea
kunyesha katika Jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumlaAlisema na kuitakia
pole sana familia yam zee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa sana
kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu katika
wakati huu mgumu kwake.Kamanda Mkumbo ametoa wito na ushauri kwa wakazi
wa Arusha kuchukuwa tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha kujenga chini
ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.
Amesema
kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga
mengine hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukuwa tahadhali
hiyo.
Aidha
kamanda ametoa tahadhari kutokana na habari za uzushizinazoendele kuwa
jana kwenye kuaga miili ya wanafunzi kuna mtu alidondoka juu ya mti na
kufariki pamoja na mama mmoja mtoto wake mdogo alifariki,amesema habari
hizo siyo za kweli wananchi wazipuuze kabisa
Mti ulioanguka ukang'ookana shina lake na kuangukia nyumba na kusababisha maafa hayo ya watu watano wa familia moja.
Jitihada za uokozi zikiendelea
Miili ikiwa imeshapakiwa ndani ya gari la polisi kwenda kuhifadhiwa hospitalini
Comments
Post a Comment