Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa 5 wa Chama cha Makatibu Mahususi
Tanzania (TAPSEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa
Jakaya Kikwete ,mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya
wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Makatibu Mahsusi
Tanzania (TAPSEA) ambao mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia)
akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala
Bora Mhe. Angela Kairuki leo kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama
Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
Chama Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewaagiza Makatibu Mahsusi nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili
na waache tabia ya kutoa siri za ofisi zao kwani kufanya hivyo ni kosa
kisheria.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa
kauli hiyo wakati anafungua mkutano wa Tano wa Chama cha Makatibu
Mahsusi Tanzania katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Mji Dodoma.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uadilifu na uaminifu ni njia pekee
ya kuaminiwa na viongozi wao hivyo ni muhimu kwa makatibu mahsusi
nchini kufanya kazi kwa bidii na ubunifu mkubwa katika maeneo yao ya
kazi.
Makamu wa
Rais pia amewahimiza makatibu mahsusi kufanya tathmini ya utendaji wao
wa kazi na wawe tayari katika kujifunza mbinu mpya za utendaji
zinazoendana na mabadiliko ya teknolojia.
“Sote
tunafahamu kuwa dunia imekuwa ni kijiji kutokana na utandawazi unaoletwa
na mifumo ya teknolojia hivyo kutokana na mabadiliko haya hamna budi
nanyi kubadilika na kwenda na wakati ili msiangaliwe kwa mtazamo hasi wa
kuwa wapiga cha tu”
Kuhusu
uanzishwaji wa Shahada ya Uhazili, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amewahakikishia makatibu mahsusi kuwa Serikali imekubali
kuanzisha shahada hiyo ambapo masomo yake yataanza mwezi wa Tisa mwaka
huu kwenye Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika mikoa ya Dar es
Salaam na Tabora.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza makatibu mahsusi kuchangamkia
fursa hiyo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu kwa kuzingatia kuwa elimu
haina mwisho.
Kwa
upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki amesema Serikali inafanyia kazi
baadhi ya kero zinazowakabili makatibu mahsusi ikiwemo kuboresha maslahi
ya kada ya uhazili nchini.
Amesema
lengo la Serikali ni kuhakikisha kada hiyo pamoja na watumishi wengine
wanapata maslahi bora ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika
kuongeza ufanisi kazi.
Comments
Post a Comment