WAZIRI MWIGULU AIONGOZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE YA ULINZI NA USALAMA KUKAGUA MRADI WA UJENZI KITUO CHA POLISI OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,
Balozi Adadi Rajabu (kushoto), akiongozana na wajumbe wengine wa kamati
hiyo wakati wakiwasili katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha
polisi, Oysterbay, leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,
Balozi Adadi Rajabu (katikati), akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika eneo la mradi
unaoendelea wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi, Oysterbay,leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba.
Mtaalamu
wa Majengo kutoka kampuni inayojenga Kituo cha Polisi Oysterbay,
Mhandisi Fanuel Malekela, akitoa maelezo ya mchoro wa ujenzi wa kituo
hicho kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya
Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (wapili kushoto),wakati kamati
hiyo ilipotembelea ujenzi wa mradi huo.Wengine ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(watatu kushoto) na Mkuu wa Jeshi la
Polisi, IGP Ernest Mangu. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Kamishna
wa Fedha wa Jeshi la Polisi, Albert Nyamhanga, akitoa maelezo ya mradi
wa Ujenzi wa kituo cha Polisi,Oysterbay kwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi
Rajabu(watatu kulia), wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mwigulu Nchemba.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba(kulia), akiwaongoza kutoka ndani
ya jengo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi
na Usalama baada ya kumaliza kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi
wa Ujenzi wa kituo cha polisi,Oysterbay leo jijini Dar es Salaam.Huku
sehemu kubwa ya mradi huo ikiwa imekamilika. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Comments
Post a Comment