KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE YA ULINZI NA USALAMA YAKAGUA MRADI WA UJENZI -OFISI ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,
Balozi Adadi Rajabu (wa kwanza kushoto), akiongozana na wajumbe wengine
wa kamati hiyo baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wa kwanza
kulia ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba
Yahaya, akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa na wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama (hawapo pichani),
wakati wajumbe hao walipotembelea mradi wa ujenzi ofisi za Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akitoa
taarifa ya mradi wa ujenzi wa ofisi za jeshi hilo kwa wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani),
wakati wajumbe hao walipotembelea mradi huo leo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rjabu na anayefuatia ni
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba
Yahaya.
Mjumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,Kapteni
Mstaafu George Mkuchika, akichangia hoja wakati wa ziara ya kamati hiyo
kukagua ujenzi wa ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es
Salaam leo.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Comments
Post a Comment