
Katibu
Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena (katikati)
akizungumza katika mkutano ana waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
kuhusu tamko la vyombo vya habari la kususia kuandika habari za matukio
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ijumaa iliyopita
alivamia kituo cha Clouds Media usiku akiwa na askari waliokuwa na
bunduki. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Dar Press Club, Shadrack Sagati
na Mjumbe wa TEF, Lillian Timbuka.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Meena
ambaye alisoma tamko la pamoja la TEF, Dare sSalaam Press Club na Umoja
wa Vilabu vya Habari nchini akijibu moja ya maswali ya wanahabari.
Jukwaa la
Wahariri Tanzania(TEF) leo limevitaka vyombo vya habari nchini
kutokuandika au kutangaza habari zozote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda.
TEF
wameyasema hayo leo katika taarifa yao na kulaani vikali kitendo cha
Makonda cha kuvamia kituo cha Utangazaji cha Clouds usiku wa Machi 17
akiwa na askari wenye silaha.
“Kwa
mantiki hiyo, tunamtangaza Ndugu Paul Makonda kuwa ni Adui wa Uhuru wa
Habari, na yeyote yule atakayeshirikiana naye katika kukandamiza uhuru
wa habari nchini,” ilisema taarifa hiyo ya TEF iliyoandikwa na
Mwenyekiti wake, Theophil Makunga.
Wanahabari wakiwa kazini
Comments
Post a Comment