Raia
takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani
saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump
atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.Wote
wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba raia hao wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu.
Bw Trump alisema Jumatano itakuwa siku muhimu kwa usalama wa Marekani.
Anatarajiwa
kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na
Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda
Marekani.
Comments
Post a Comment