Rais Barack Obama amewaaga Wamarekani na ulimwengu
mzima kwa mara ya mwisho akiwa kama rais, katika hotuba iliyojaa hisia
kubwa aliyoitoa mjini Chicago na kuwataka Wamarekani kuunganisha nguvu
katika kuleta mabadiliko.
Rais Barack Obama amewaaga Wamarekani na ulimwengu
mzima kwa mara ya mwisho akiwa kama rais, katika hotuba iliyojaa hisia
kubwa aliyoitoa mjini Chicago na kuwataka Wamarekani kuunganisha nguvu
katika kuleta mabadiliko.
Akihitimisha utawala wake katika Ikulu ya Marekani, Obama amerejea katika mji ambao sasa ni nyumbani kwake wa Chicago ambako kampeni yake ya "ndio tunaweza" ilianzia hapo na leo akisema "ndio tumeweza".
Mafanikio aliyoyapata
Akiorodhesha mafanikio ya utawala wake kuanzia mkataba wa nyukilia na Iran hadi huduma ya bima ya afya, sehemu kubwa ya hotuba yake iliegemea katika kuwatia moyo wafuasi wake waloshutushwa na ushindi wa Donald Trump pamoja na kutathmini mafanikio aliyoyapata katika uongozi wake na mtazamo wake kuhusu wapi Marekani inaelekea .
Obama amewataka Wamarekani kuamka, kupigania demokrasia lakini akaonya kuwa ubaguzi wa rangi na kukosekana kwa usawa bado ni kitisho kwa demokrasia. "Sisi sote bila ya kujali vyama, ni lazima turudi katika ujenzi wa taasisi ya demokrasia", amesema Obama.
Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden anayemaliza muda wake
Miiongoni mwa mafanikio mengine anayojisifia kwayo Obama ni pamoja na kuimarishwa kwa uchumi, kuhalilisha ndoa za jinisia moja, kufunguliwa kwa mahusiano ya kidiplomasia na Cuba na maenedeleo mengine.
Mke wake Michele Obama na makamu wa rais Joe Biden na mke wake Jill ambao rais amewaelezea kama "familia" wamehudhuria hafla hiyo.
Ashindwa kujizuia
Rais Barack Obama akiwa na watoto wake Malia na Sasha mjini Washington
Anasema Marekani imekua bora na yenye nguvu duniani tangu alipokula kiapo kuiongoza nchi hiyo miaka nane iliyopita. Donald Trump atakayeapishwa Januari 20 anatarajiwa kuondoa baadhi ya yaliyofikiwa na karibu kiasi ya watu elfu 18 waliohudhuria hafla hiyo mjini Chicago walimshangilia rais huyo wakisema "miaka minne zaidi" na Obama akasema hawezi kufanya hivyo.
Obama katika hotuba yake ya mwisho ameepuka kumkosoa Trump moja kwa moja na kulaani mgawanyiko ambao umezikumba siasa za taifa hilo.
Mwandishi: Sylvia Mwehozi /AFP
Mhariri: Iddi Ssessanga
Comments
Post a Comment