Muonekano wa Mgodi wa Buzwagi katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa ameuongoza
ujumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini ili
kukagua na kuhoji utendaji na ushiriki wa mgodi wa Buzwagi katika
masuala ya kijamii mkoani Shinyanga hivi karibuni.
Katika
ziara hiyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeutaka
Uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kuwashirikisha wananchi pamoja na
wafanyakazi wa Mgodi huo Mpango wa kuufunga Mgodi huo (Mining Closure
plan) unaotarajia kufunga shughuli zake za uzalishaji wa Dhahabu ifikapo
Desemba 2017, huku shughuli za uchejuaji zitaendelea kwa miaka miwili.
Hoja hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Doto Mashaka Biteko mara baada ya kuwasili na kukutana na uongozi wa mgodi huo wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa mgodi huo.
Biteko
alisema kuwa Wananchi na wafanyakazi lazima wawe sehemu ya ufungaji wa
Mgodi huo kwa kuwa jambo hilo ni kubwa kwani litatikisa Uchumi wa
wananchi wa Kahama na pia Halmashauri ya Kahama itakosa Ushuru wa Huduma
ambazo Mgodi huo umekuwa ukilipa kila mwaka.
“Mgodi
huo unalipa Ushuru wa Huduma kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama na
wafanyakazi katika mgodi huo wana ajira kwa hiyo mipango ya kufunga
mgodi huo iwe sehemu ya wananchi kwa asilimia mia” alisisitiza Biteko.Aidha
Biteko alitaka ufafanuzi zaidi kutoka kwa Uongozi wa Mgodi huo ni
sababu zipi zinazopelekea mgodi huo kufungwa. Vilevile, alitaka Uongozi
kuijulisha kamati hiyo jambo ambalo mgodi huo unawaachia wanannchi wa
Kahama mara baada ya shughuli za uzalishaji kufungwa.
Akijibu
hoja hizo Meneja wa Mgodi wa Buzwagi, Assa Mwaipopo alisema kuwa
Serikali na wananchi wamekuwa wakishirikishwa kikamilifukakita shughuli
mbalimbali za mgodi huo ikiwemo kuhusu nini kifanyike baada ya kufunga
mgodi. Alieleza kuwa, Mgodi na Serikali wanansubiri maoni ya wananchi
kuhsu shughuli sahihi za kufanya katika eneo hilo la mgodi mara tu
utakapomaliza shughuli zake.
Mwaipopo
alifafanua kuwa ingawa mgodi umekuwa ukipata faida kutokana na
shughuliza uchimbaji dhahabu bado mgodi haujarudisha gharama za awali
ambazo zilitumika wakati wa uwekezaji huo.
Akijibu
swali la mjumbe mwingine wa kamati ya Bunge aliyehoji juu ya malalamiko
ya wafanyakazi wa mgodi huo kutokujua mwajiri wao kwa kuwa mikataba yao
inaonesha ni kati yao na Pangea Mining Gold, vitabulisho vyao vinatoka
African Barrick Gold Mine na malipo yao yanaonesha yanalipwa na Acacia
Mining Gold. Mwaipopo alisema kuwa mmiliki wa Mgodi huo ni Pangea na
ndiye anayewajibika na huyo ndiye mwaajiri wao.
Aidha
Kamati ya Kudumu ya Wizara ya Nishati na Madini iliitaka Wizara kutoa
ufafanuzi wake ni kwa nini Mgodi wa Buzwagi unaendelea kubadili majina
kama vile Pangea, African Gold Mine na Acacia Gold Mine.
Akitoa
ufafanui wa suala hilo, Kaimu Kamishna wa Madini, Ally Samaje alisema
kuwa mgodi unapobadili jina au anwani basi haina madhara lakini pale
unapobadili umiliki wake, lazima mchakato huo wote ushirikishe serikali
na upate ridhaa ya serikali kwa kuwa hapo kuna ulipaji wa Kodi na Mapato
mbalimbali kwa serikali.
Ziara hii
ni wiki moja inayowawezesha wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Wizara ya
Nishati na Madini kukagua na kuhakikisha wizara wanazozisimamia
zinatekeleza majukumu yao kama inavyowapasa.
Comments
Post a Comment