
Msemaji
wa shirika hilo, Danyal Gilani alisema ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria
30 na wengine waliosalia wakiwa wahudumu na marubani.
Katika
taarifa yake shirika hilo lilisema ndege hiyo ilikuwa imebeba watu
‘wanaokadiriwa kuwa 40’ lakini taarifa kutoka mamlaka ya anga ilisema
kulikuwa na watu 47. Ofisa mwandamizi wa polisi, Laiq Shah alisema ndege
hiyo ilianguka katika eneo linalofahamika kama Haveliana.
“ Timu ya
waokoaji imeelekea kwenye eneo la tukio nadhani baada ya hapo tutapata
taarifa zaidi,” alisikika akieleza msemaji wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege, Pervez George wakati akizungumza na Reuters.
Maofisa
wa polisi katika eneo hilo waliiambia televisheni ya taifa kuwa ndege
hiyo ilianguka katika kijiji kimoja kilichopo kaskazini mashariki mwa
Pakistan.
Shirika
la habari la AP liliarifu kuhusu kundi la waokoaji kuelekea kwenye eneo
la tukio. Moshi mkubwa ulishuhudiwa ukivuka toka eneo ambalo ndege hiyo
ilianguka. Imeelezwa kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano dakika 90
tangu ianze kuruka.
Comments
Post a Comment