RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NA JAMHURI YA KOREA HAPA NCHINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young mara baada ya
kupokea picha hiyo ya mfano wa Daraja jipya la Salenda.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
kumkaribisha Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov aliyefika Ikulu
kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na
Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov mara baada ya kumaliza mazungumzo
yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
kumkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young
aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea picha
ya mfano wa Daraja jipya la Salenda litakojengwa kuanzia maeneo ya
Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini hadi eneo la Coco beach
jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song
Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Daraja hilo litakuwa
na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini
na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza
maelezo kuhusiana na ujenzi wa daraja hilo jipya la Salenda kutoka kwa
Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Comments
Post a Comment