Riasi Magufuli ahutubia wananchi wa Gieta Mjini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Geita mjini mara baada ya kuwasili kutoka Kahama.
RAIS John Pombe Magufuli, ameagiza masalia ya mawe yanayotokana na uchimbaji dhahabu kwenye mgodi wa kuchimba dhahabu wa Geita Gold Mine, maarufu kama "Magwangala", wapewe wananchi wa eneo hilo la Geita.
Rais alitoa agizo hilo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Geita mjini wakati alipowasili mjini humo akitokea wilayani Kahama, katika ziara yake aliyoianzia mkoani Dodoma.
"Natoa wiki tatu, mchakato wa kuyagawa Magwangala uanze mara moja, naagiza NEMC kwa kushirikiana na taasisi nyingine, waanze utaratibu wa kuyagawa magwangala mara moja, na asije akajitokeza mtu kuzuia agizo langu," rais alisema.
Rais Magufuli alisema, Dhahabu ni ya watanzania, na kama isingekuwepo hao wanaozuia wasingeweza kufanya hivyo, " Lakini nawaomba ndugu wananchi, zoezi hilo litakapoanza, lianze kwa utaratibu bila ya kuleta madhara." Rais alishauri.
Swala la magwangala kugawiwa kwa wananchi limekuwa likileta mvutano mkubwa na kwa kiasi fulani swala hilo lilitaka kuathiri kampeni za CCM mkoani Geita hadi makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alipowaahidi wananchi kuwa serikali itahakikisha swala hilo linapatiwa ufumbuzi na serikali kwa haraka iwezekanavyo.


 Wananchi wakishangilia hotuba ya Rais.
Rais Magufui akiwapungia mkono wananchi wakati akiwasili Geita mjini.

Comments