UFUNGUZI WA KANISA LA PAROKIA YA EKARISTI MTAKATIFU- KABUHIMA-JIMBO LA KAHAMA




Picha ya Kanisa linalokwenda kufunguliwa na Askofu Mkuu Francisco Padilia (Balozi wa Papa mtakatifu-Tanzania)




 Picha ya Askofu Mkuu Francisco Padilia (Balozi wa Papa mtakatiu nhiniTanzania) akikata utepe katika mlango wa Kanisa

Mwonekano wa ndani wa Kanisa la Parokia ya Ekaristi Takatifu-Kabuhima






Picha ya(mwenye joho jeupe) aliyekuwa msimamizi wa Parokia talajiwa Padre Slivatory Guerrera ametawaza rasmi na Askofu wa Kanisa la Katoliki Jimbo Kuu la Kahama Ludovick  Minde
kuwa msimamizi Mkuu wa Parokia ya  ekaristi takatifu mbele ya Askofu mkuu Francisco Padillia barozi wa papa  Tanzania, aliyekuwa mgeni rasmi kutabalukiwa kanisa la ekaristi takatifu “Kabuhima” lililopo kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita. Askofu Minde aliwaomba waumini kumpa ushirikiano Paroko Guerrera ili aendelee kumtumikia Mungu.

 

Mhasibu wa Parokia hiyo Elizabeth Mathiasi(Kulia) akisoma risala ya Parokia siku ya kutabarukiwa kanisa hilo na kutawazwa rasmi Paroko Guerrera awali alisema asili ya Parokia hiyo ni Kigango cha Lyobahika kiliazishwa 1936 kutoka kigango cha Ushirombo ikiwa baado Jimbo la Tabora.
Mathiasi alisema 2003 Askofu Jimbo la Kahama Minde kutokana na fikira za kiuchungaji aliona vema kuazisha Parokia nyingine aliitangaza rasmi Novemba 8 mwaka 2003  na kuipa jina la ekarist takatifu Kabuhima ikisimamiwa na Padre Guerrera.
Pia mhasibu Mathiasi aliwakumbuka wapendwa wafadhiri wa  kubwa katika kujenga kanisa  na kwa sasa walishatangulia mbele zahaki Sopiatia Mkulla,Charle Kulwa,Mzee Mourice Kapella,na mwingine Domian Shirima wanawaombea kwa mungu aziweke roho zao mahali pema peponi.




Barozi wa papa Padillia akihutubia maelfu ya waumini wa kanisa hilo alisema “Leo hii tunashuhudia tukio muhimu katika Jimbo la Kahama, kubariki kanisa zuri Ekarist takatifu kwanza na kumpongeza sana baba askofu Ludovick Minde na Mapadri watawa na waumini wote kwa majitoleo yao kwa kulijenga kanisa zuri namna hii”.
“kwa kipindi hiki cha Pasaka tunaimba haleluya asifiwe Mungu na bwana wetu Yesu Kristo  kwa matendo asifiwe kwa sehemu hii nzuri ya kuabudiwa itawapa fursa wanaparokia kumuomba Mungu na kumuabudu kumushukuru kwa Baraka zake nyingi hivyo  moyo wa ibada na amani vitawale ndani ya waumini wa parokia hii”.
Padillia alisema kupitia ibada hii ya kutabalukiwa kanisa la Parokia inanilazimu kukumbusha yale ambayo baba mtakatifu aliyasema siku na wakati anaombea amani duniani alisema shughuli za kisiasa na kiuchumi haziwezi kuchukuliwa katika mantiki ya kufahamu kufanya mambo bila kuendeshwa na mwanga wa mungu.


Comments