Bonanza la Tigo kubamba Mji wa Ushirombo

 Vinara wa mchezo kati ya Young Boys Vs Carpenter Fc


 Kama kawaida ya mashabiki kuonyesha hisia zao.
 Timu ya Young Boys Fc Vs Carpenter zikitoka uwanjani baada ya mechi kumalizika huku pakiwa na mvua kubwa.
 Timu ya Mount City Vs Young Boys Fc zikiwa tayari kwa ukaguzi ilizianze mechi ya Fainali ya Bonanza hilo la Tigo.

 Timu ya Young Boys Fc Vs Mount City Fc wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi walioandaa Bonanza hilo la Tigo kabla ya mechi kuanza
 Muonekano wa Meza Kuu.


 Mwenyekiti wa Chama Mpira BUFA Bw. Maganga akizungumza na wadau mpira baada ya mashindano ya Bonanza kumalizika.


  Kiongozi na mchezaji wa Timu ya Ushirombo Rangers akipokea zawadi ya T-Shirt kwa niaba ya mchezaji mwenzake Anthony Mwayoyo kwa kuwa na nidhamu mchezoni
 Mchezaji wa Timu ya Young Boys Fc Gaspar akipokea zawadi ya T-Shirt ya Kampuni ya Tigo baada ya kuwa mchezaji bora.
 Goli kipa wa Timu ya Carpenter akipokea zawadi ya Golikipa Bora wa Bonanza
Timu ya Young Boys Fc wakiwa katika shamlashamla za ushindi.


Timu ya Young Boys Fc iliibuka kidedea baada ya kuichapa  gori 3-2 timu ya Mount City Fc kupitia mikwaju ya penaliti baada ya kutoka sare ndani ya dakika tisini za mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Ushirombo  Wilayani Bukombe Mkoani Geita

Katika mchezo huo uliofadhiliwa na Kampuni ya Tigo ulizijumuisha timu nne ambazo ni Ushirombo Rangers Fc,Carpenter Fc,Mount City Fc na Young Boyz Fc na kushindania zawadi ya kiasi cha shilingi elfu  50 na pea moja ya jezi yenye thamani ya  laki moja kwa mshindi wa kwanza na mshindi wa pili shilingi elfu 75 wa tatu elfu 50 nawa nne akipata elfu 25, Timu ya Young Boys Fc ilifanikiwa kunyakua zawadi hiyo nono baada ya kuichapa gori 3-2 timu ya Mount City fc na nafasi ya mshindi wa tatu ikishikiliwa na Timu ya Carpenter Fc. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo mdhamini wa Bonaza hilo Madame Ida alisema bonaza hilo ni kwa ajili ya vijana wanaopenda kucheza mpira wa miguu  ambapo ameamua kushindanisha timu nne huku akiwasihi wazidi kujitokeza mara kwa mara katika mabonza mengine ya Kampuni ya Tigo ili kukuza vipaji vyao na kumuunga mkono kwani yeye anapenda sana michezo.

Kwa upande wao baadhi ya mashabiki wa timu hizo Siza Manota  na Baraka Mangabe wamesema wamefurahishwa sana na mechi zote na kuwataka Timu zingine kukazabuti iliziweze kufanya vizur kama Young Boys FC katika Mechi za leo.


Comments