Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wamejitokeza kwa wingi kushuhudia fainali ya mashindano ya KNK CUP 2026, yaliyoandaliwa na kudhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko, katika kuadhimisha miaka 10 tangu achaguliwe kuwa Mbunge wa jimbo hilo mwaka 2016.
Mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka chini ya udhamini wa Dkt. Biteko, yakilenga kukuza na kuibua vipaji vya vijana kupitia michezo, pamoja na kuimarisha mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wananchi wa Bukombe.
Fainali ya mwaka 2026 iliyofanyika Septemba 7, 2026, ilizikutanisha timu za Ushirombo Warriors FC na Katome FC, ambapo Ushirombo Warriors FC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, na kutawazwa kuwa mabingwa wa KNK CUP 2026 kati ya timu 248 zilizo shiliki mashindano hayo.
Baada ya ushindi huo, Ushirombo Warriors FC ilikabidhiwa zawadi ya ubingwa, huku wachezaji, viongozi na mashabiki wakisherehekea mafanikio hayo.
Mamia ya wananchi waliohudhuria fainali hiyo walisema tukio hilo lilikuwa zaidi ya mchezo wa soka, bali lilikuwa sehemu ya kusherehekea miaka 10 ya mafanikio na mchango wa Dkt. Biteko katika maendeleo ya michezo na jamii ya Bukombe.
Wananchi hao walieleza kuwa mashindano hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuibua vipaji vya vijana, kuwapa fursa ya kushiriki michezo na kuwaunganisha wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bukombe.
Aidha, walitaja ujenzi wa uwanja wa Bukombe Stadium kuwa moja ya hatua muhimu katika maendeleo ya michezo wilayani humo, wakisema uwanja huo unatoa mazingira bora zaidi kwa vijana na timu mbalimbali kuendeleza vipaji vyao.
Akizungumza wakati wa fainali hiyo, mmoja wa wananchi, Thomas Shija, alisema Dkt. Biteko ni kiongozi anayelenga kuiona Bukombe ikipiga hatua katika nyanja mbalimbali, ikiwemo michezo na uchumi.
“Mbunge wetu ni kiongozi anayeiwazia mema Wilaya ya Bukombe. Tunaona maendeleo katika nyanja mbalimbali, ikiwemo michezo, na mashindano haya yamekuwa chachu ya kuibua vipaji vya vijana,” alisema Shija.
Kwa upande wao, mashabiki na wadau wa michezo walieleza matumaini yao kwamba KNK CUP itaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuibua vipaji vipya vitakavyoweza kuwakilisha Bukombe katika ngazi za juu za mashindano ya soka nchini.
Fainali hiyo imehitimisha kwa shangwe kubwa, huku wananchi wakitumia siku hiyo kama sehemu ya kusherehekea miaka 10 ya KNK CUP ya na Kusema na Kutenda na mchango wa mashindano hayo katika kukuza michezo na vipaji vya vijana wa Bukombe.
Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhadis Paskas Mragili alisema uwanja huo unauwezo wa kubeba watu 5000 mzunguko wa viti ukiodoa mzunguko na Mbunge amekuwa akidhamini mashindano kila mwaka na imekuwa ikiwafanya vijana wengi kuinekana na kuchukuliwa na timu za madaraja ya juu.

Comments
Post a Comment