Na, Ernest Magashi
Mwenge wa Uhuru 2026 umeingia mkoani Geita na kuanza rasmi mbio zake za kuhamasisha maendeleo, uzalendo, amani, umoja na mshikamano katika mkoa huo.
Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yamefanyika leo, Agosti 24, 2026, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nyah'wale mkoani Geita, baada ya mwenge huo kuwasili ukitokea mkoani Shinyanga
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Martine Shigela, amesema Mwenge wa Uhuru utakapokuwa mkoani Geita utakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo miradi 42 yenye thamani ya shilingi bilioni 168.7.
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita wamejitokeza kwa wingi kushiriki mapokezi hayo, wakionesha uzalendo, mshikamano na shauku ya kuupokea Mwenge wa Uhuru unaoendelea na mbio zake katika maeneo mbalimbali nchini.
Mapokezi hayo yameambatana na shughuli mbalimbali za kijamii, burudani pamoja na ujumbe wa maendeleo unaolenga kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, huku wakisisitizwa kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa.

Comments
Post a Comment