MAJERUHI YAWANYIMA FURSA YA KUNG'ARA KNK CUP 2026

Na Ernest Magashi

ebukombesasablogspot.com.tz

Baadhi ya wachezaji waliokuwa wakitajwa kuwa miongoni mwa watakaong'ara katika mashindano ya KNK Cup 2026 wamejikuta wakikosa nafasi ya kushiriki kutokana na majeraha yaliyowakumba kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, hali iliyowavunja moyo na kuwanyima fursa ya kuonyesha vipaji vyao pamoja na kujiongezea kipato.Miongoni mwao ni kiungo wa Bukombe Veterans, Gaspa Lukas (26), ambaye anasumbuliwa na jeraha la kifundo cha mguu wa kushoto alilolipata wakati akicheza mechi ya kulipwa, muda mfupi kabla ya kuanza kwa KNK CupAkizungumza na mwandishi wa Bukombe Sasa Media kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Ushirombo, Gaspa alisema maumivu makubwa kwake si jeraha pekee, bali ni kushuhudia wenzake wakishiriki mashindano huku yeye akibaki nje ya uwanja."Nilikuwa nimejiandaa vizuri kushiriki KNK Cup mwaka huu na kuongeza kipato kupitia soka. Bahati mbaya nilipata jeraha, na daktari amenitaka nipumzike kwa miezi miwili na wiki moja. Hivyo, mashindano yatakuwa yamekwisha kabla sijapona," alisema Gaspa.Mbali na Gaspa, mchezaji mwingine Raban Henry anayefahamika kwa jina la Shana Kamsoko pia ameshindwa kushiriki KNK Cup 2026 kutokana na majeraha yanayoendelea kumuweka nje ya uwanjaNaye nyota wa soka wa mitaa ya Kilimahewa, maarufu kwa jina la Mambo Mambo, alionekana akifuatilia fainali ya KNK Cup katika Kata ya Bulangwa Uhirombo Warrions wali ibuka mabigwa zidi ya Ashanti FC akiwa anatumia gongo la kutembelea kufuatia jeraha la mguu wa kuliaMambo alisema bado yuko kwenye matibabu na hataweza kucheza msimu huu wa KNK Cup, licha ya kutamani kushiriki mashindano hayo ambayo amesema humsaidia kukuza kipato na kuendeleza kipaji chake cha soka.Majeraha hayo yamewakatisha ndoto wachezaji hao kushiriki moja ya mashindano makubwa yanayovuta hisia za wananchi wa Wilaya ya Bukombe, huku mashabiki wakisubiri kuwaona wakirejea uwanjani wakiwa na afya njema katika msimu ujao.

Comments

  1. Mwenyezi Mungu aendelee kuwaponya majeraha yao,BUKOMBE (KNK)

    ReplyDelete

Post a Comment