KATENTE UNITED YAING'OA KIGOS RANGERS 1-0, YATINGA FAINALI YA KNK CUP 2026 KATA YA KATENTE

Na, Ernest Magashi

ebukombesasablogspot.com.tz

Katente United FC imefanikiwa kutinga fainali ya mashindano ya KNK Cup 2026 ngazi ya Kata ya Katente baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Kigos Rangers FC katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Michezo wa Katente.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Avani Nzonzi dakika ya 38, bao lililowatosha Katente United kukata tiketi ya kucheza fainali ya kata huku likiiaga Kigos Rangers FC kwenye mashindano ya mwaka huu.

Kipindi cha pili Kigos Rangers FC waliongeza kasi ya mashambulizi wakisaka bao la kusawazisha, lakini walikwama mbele ya safu imara ya ulinzi ya Katente United iliyodhibiti vyema mashambulizi yote hadi mwamuzi alipopuliza kipenga cha mwisho.Akizungumza baada ya mchezo huo Julia 18,2026, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Katente ambaye pia ni msimamizi msaidizi wa mashindano ya KNK Cup 2026, alimpongeza mdhamini wa mashindano hayo, Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt. Doto Biteko, kwa kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo imekuwa jukwaa muhimu la kuibua vipaji vya vijana na kuhamasisha maendeleo ya soka katika wilaya ya Bukombe.Kwa ushindi huo, Katente United sasa inajiandaa na mchezo wa fainali ya kata ikiwa na matumaini ya kutwaa ubingwa na kufuzu hatua inayofuata ya mashindano ya KNK Cup 2026.

Comments