MRADI WA KUSAFRISHA UMEME CHALINZE, DODOMA KUKAMIRIKA AGOSTI MWAKA HUU.


Na, Ernest Magashi

ebukombesasa.blogspot.com.tz

Mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Zuzu, Dodoma, unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 18, 2026.Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, alisema hayo leo Mei 20, 2026 wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo katika mikoa ya Morogoro na Dodoma.Twange alisema mradi huo ni muhimu kwa kuwa unasafirisha umeme unaozalishwa moja kwa moja kutoka katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere ambao unapita Chalinze hadi Dodoma.Alisema utekelezaji wa mradi huo unaenda sambamba na upanuzi wa vituo vya kupokea na kupoza umeme vya Chalinze na Zuzu, Dodoma, ambapo kukamilika kwake kutaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwa ajili ya shughuli za uwekezaji pamoja na kuongeza fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi nchini.Twange aliongeza kuwa Serikali Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Shilingi bilioni 514 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo ambao utachochea shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kuendana na kasi ya ongezeko la mahitaji. 

Comments