MNEC GEREVAS AMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA NA DKT. BITEKO KWA MAENDELEO BUKOMBE


Na, Ernest Magashi

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Gerevas, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwaletea wananchi wa Wilaya ya Bukombe na Watanzania kwa ujumla fedha za maendeleo zinazochochea ustawi wa jamii.Gerevas alitoa pongezi hizo wakati akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM iliyofanyika kimkoa katika Kata ya Namonge, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.Akiwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, aliwataka wanachama wa Jumuiya ya Wazazi pamoja na jumuiya nyingine za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuwaunga mkono madiwani pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko, huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kumpa ushirikiano Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.“Maendeleo yote yanayoonekana Bukombe, ikiwemo fedha zaidi ya shilingi bilioni 11 zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Rais Dkt. Samia na Dkt. Biteko. Niwaombe wananchi na wanachama wa CCM kuendelea kuwaunga mkono viongozi wetu,” alisema Gerevas.Alisema fedha hizo zimeelekezwa katika kuboresha huduma za afya, elimu pamoja na sekta nyingine muhimu za maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Bukombe.Aidha, Gerevas aliwataka viongozi wa chama kuanzia ngazi ya tawi, hususan Jumuiya ya Wazazi, kuacha kulalamika na badala yake kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi kupitia vikao vya ndani kwa kushirikisha watalamu. Pia alisisitiza umuhimu wa malezi bora kwa watoto kwa kuzingatia maadili ya Kitanzania ili kusaidia kupunguza vitendo vya uhalifu miongoni mwa vijana.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Bukombe, Hassan Mohamed, alisema wanajivunia uwepo wa viongozi makini ndani ya chama ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa mafanikio makubwa.Mohamed alisema jumuiya hiyo inatarajia kuanzisha mradi mpya baada ya kupata eneo la uwanja, huku wakihitaji kiasi cha shilingi milioni saba kwa ajili ya utekelezaji wake. Alisema MNEC Gerevas alichangia shilingi milioni mbili na kuongoza harambee ya kuchangisha fedha za kukamilisha mradi huo.Awali, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita, Philibert Ngemela, alisema viongozi wa jumuiya hiyo wanaendelea kufanya ziara mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha ulipaji wa ada za wanachama, kuimarisha uhai wa jumuiya pamoja na kuazisha na kuendeleza miradi ya kiuchumi.Akitoa shukrani kwa MNEC Gerevas kwa mchango wake katika maendeleo ya jumuiya hiyo, Ngemela alisema Jumuiya ya Wazazi inamiliki eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 3,964 kwa ajili ya kuanzisha mradi wa mafunzo ya ufundi stadi (VETA) ngazi ya mkoa.Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Erick Kagoma alisema kuwa halmashauri imepokea zaidi ya shiringi bilioni 11 toka Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 

Comments