KAMATI YA USALAMA WILAYA YAANZA KUKAGUA MIRADI ITAKAYO PITIWA NA MWENGE WA UHURU 2026

Na, Ernest Magashi

ebukombesasa.blogspots.co.tz.

Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imeanza kukagua miradi ya maendeleo itakayo pitiwa kukaguliwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru mwaka 2026.kamati hiyo ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, mhadisi Paskasi Muragili, waliungana na wataalamu kutoka idara mbalimbali za Halmashauri. Mhadisi Muragili alisema Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 utapitia miradi ya maendeleo na tumeaza kuzikagua kwa lengo la kujionea hatua za utekelezaji, ubora wa kazi pamoja na kuhakikisha miradi hiyo inakidhi vigezo vinavyotakiwa kabla ya kupitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Katika ukaguzi huo kamati ilitembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuendelea kuboresha huduma za kijamii na kuinua uchumi wa wananchi.Aidha Miradi iliyotembelewa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Sekondari Ushirombo, ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe. Pia walikagua ujenzi wa Zahanati ya Igulwa, ujenzi wa barabara ya Igulwa, mradi wa maji Buntubili, Businda, kikundi cha vijana Mwembeni Furniture, kikundi cha Bora Maziwa, pamoja na mradi wa nishati safi na salama ya kupikia.Mhadisi Muragili alisisitiza watalamu wanaosimaimia miradi yote wahakikishe inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na kutoa huduma zenye tija kwa wananchi.Aidha aliwaagiza wataalamu wanaosimamia miradi hiyo kuongeza usimamizi ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta matokeo yaliyokusudiwa.Kwa upande wao wataalamu wa Halmashauri kwa nyakati tofauti waliimbia kamati ya usalama kuwa hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi maandalizi yanaendelea vizuri ili kuhakikisha miradi inakuwa tayari kupitiwa na Mwenge wa Uhuru.

Comments