DKT. BITEKO AWAPONGEZA WAUGUZI BUKOMBE KWA HUDUMA ZA KUOKOA MAISHA YA WANANCHI

Na, Ernest Magashi

ebukombesasa.blogspot.com.tz

Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita na Naibu Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Doto Biteko, amewapongeza wauguzi wilayani Bukombe kwa kazi kubwai wanayoifanya ya kuokoa maisha ya wananchi kupitia huduma wanazotoa katika vituo mbalimbali vya afya.Pongezi hizo alizitoa wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ngazi ya wilaya, yaliyofanyika katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Bukombe katika hafla ya usiku maalum kwa wauguzi.Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Biteko alisema anatambua mchango mkubwa wa wauguzi na madaktari katika utoaji wa huduma za afya, jambo ambalo limepunguza malalamiko ya wananchi kuhusu huduma hizo katika ziara zake za vijijini.Dkt. Biteko alisema kufatia Siku ya waunguzi duniani 2026 wilaya ya Bukombe yenye kaulimbi isemayo "wauguzi Wetu, Mstakabali Wetu. Wauguzi Waliowezeshwa Huokoa Maisha" Aidha, alisema Kwa  kushirikiana na Serikali atafanyia kazi bazi ya changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wauguzi kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mhandisi Paskas Muragili, ikiwa ni sehemu ya kuthamini na kutambua mchango wao katika sekta ya afya ikiwa serikaki makini inayo ongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaedelea kujali watumishi wa umma wakiwemo wa afya."Nawapongeza sana wauguzi kwa kazi kubwa mnayoifanya. Natambua mchango wa wauguzi na madaktari katika kuwahudumia wananchi. Hata katika ziara zangu za vijijini, maswali na malalamiko kuhusu huduma za afya yamepungua tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Leo mnaposherehekea usiku huu maalum, ni ishara kuwa wananchi wanatambua kazi nzuri mnayoifanya," alisema Dkt. Biteko.Kwa upande wake, Muuguzi Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Diana Makubi, akizungumza kwa niaba ya wauguzi, alisema wataendelea kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto za wateja kupitia madawati yaliyopo katika vituo vya kutolea huduma za afya.Alisisitiza kuwa wauguzi wataendelea kufanya kazi kwa weledi na kujenga mahusiano mazuri kati ya wahudumu wa afya na wananchi ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma.

 

Comments