HALMASHAURI YA BUKOMBE YAPOKEA BILIONI 18 KWA MIRADI YA MAENDELEO

Na, Ernest Magashi

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita imepokea shilingi bilioni 18 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya na maji, barabara.Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, Erick Kagoma, wakati wa ziara ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Dkt. Doto Biteko, akiwa katika ziara yake, aliwashukuru wanachama na wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge na mwakilishi wao, pamoja na kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani.Aidha, Dkt. Biteko alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka fedha za miradi ya maendeleo, na kuwataka wanachama na wananchi kuendelea kumuunga mkono kwa mshikamano na upendo, ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta manufaa kwa jamii.Alisema Rais Samia ana maono makubwa kwa taifa, ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo, wakiwemo wakazi wa Bukombe. Hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kumuombea ili mipango yake iweze kutimia kikamilifu.Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Uyovu, Mathayo Kagoma, alimshukuru mbunge kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya eneo hilo. Pia aliomba kufikisha salamu kwa Rais Samia, akieleza kuwa wananchi wanampenda na wanaendelea kumuombea.


Comments