Rais wa Klabu ya Espérance de Tunis ya nchini Tunisia, Hamdi Meddeb, amemfuta kazi Kocha Mkuu wa timu hiyo, Maher Kanzari, kufuatia kipigo cha bao 1–0 walichopata dhidi ya Stade Malien jana, matokeo yaliyoihatarisha nafasi ya klabu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Hatua hiyo imekuja licha ya Kanzari kuiongoza Espérance kupata jumla ya alama nne dhidi ya Simba SC, huku wakivuna alama mbili pekee dhidi ya wapinzani wengine katika hatua ya makundi.
Kwa sasa, Espérance de Tunis inakabiliwa na mtihani mgumu katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Petro Atlético, ambapo italazimika kuepuka kipigo ili kuhakikisha inafuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika

Comments
Post a Comment