MAONO YA DKT. SAMIA YATEKELEZWA KWA VITENDO BUKOMBE: CCM YAKAGUA UJENZI WA MAABARA SHULE YA SEKONDARI NGA’NZO
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bukombe kimetembelea Shule ya Sekondari Nga’nzo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi ambazo ni Chemistry, Biology na Physics, ikiwa ni utekelezaji wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha sekta ya elimu nchini.
atika ziara hiyo, viongozi wa CCM Wilaya ya Bukombe walipata fursa ya kujionea hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa maabara hizo, ambapo walieleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo pamoja na ubora wa kazi unaoendelea kufanyika.
Viongozi hao walisisitiza kuwa ujenzi wa maabara hizo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya sayansi ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Aidha, walitoa wito kwa walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla kuendelea kushirikiana na Serikali katika kulinda na kutunza miundombinu ya elimu mara itakapokamilika, ili iweze kuleta manufaa ya muda mrefu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Ziara hiyo ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali, ikiwa ni dhamira ya kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.



Comments
Post a Comment