Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Bulangwa jana kimeadhimisha miaka 49 tangu kuzaliwa kwa chama hicho kwa kufanya shughuli ya upandaji miti katika Shule ya Sekondari Bulangwa, ikiwa ni sehemu ya kuenzi maadili ya uzalendo, utunzaji wa mazingira na maendeleo endelevu.
Katika maadhimisho hayo, wanachama wa CCM kata hiyo pamoja na viongozi mbalimbali walikusanyika shuleni hapo na kushiriki zoezi la kupanda miti, wakisisitiza umuhimu wa kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo, sambamba na sera na miongozo ya chama pamoja na serikali.
Mbali na shughuli ya upandaji miti, kikao maalum kilifanyika ambapo walijadili mafanikio mbalimbali yaliyopatikana nchini Tanzania tangu kuanzishwa kwa CCM, yakiwemo maendeleo katika sekta za elimu, afya, miundombinu, uchumi na utawala bora.
Viongozi wa chama walieleza kuwa maadhimisho ya miaka 49 si tu kusherehekea historia ya CCM, bali ni fursa ya kutathmini safari ya chama, mafanikio yake na kuweka mikakati ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na uwajibikaji.
Maadhimisho hayo yalihitimishwa kwa wito kwa wanachama na wananchi kuendelea kushikamana na chama, kulinda amani na kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazotekelezwa na serikali kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.
![]() |










Comments
Post a Comment