MBUNGE (MNEC) DKT. BITEKO AHUDHURIA KIKAO CHA BARAZA KUU LA WAZAZI CCM TAIFA


Na, Ernest Magashi

Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (MNEC), Dkt. Doto Biteko, ameudhuri­a Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kilichofanyika leo Januari 17, 2026.Dkt. Biteko alionekana akiwa na furaha pamoja na wajumbe wenzake mara baada ya kuingia katika ukumbi wa kikao hicho muhimu, ambacho kinalenga kuimarisha mshikamano, maadili na mchango wa wazazi katika kukijenga na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi pamoja na Taifa kwa ujumla.

Kauli mbiu ya kikao hicho “Wazazi Imara, CCM Imara Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.”

Comments